Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Jamhuri Ya Kidemokrasia Ya Kongo (Kinshasa)
    2004 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehovah
    • Mbali na kushughulikia matatizo nchini humo, ofisi ya tawi ya Kongo iliwatunza pia Mashahidi wakimbizi kutoka nchi jirani ya Angola na Sudan. Huko kaskazini-mashariki mwa Kongo, Zekaria Belemo, ambaye alikuwa mwangalizi anayesafiri wakati huo, alitembelea kikundi cha ndugu wakimbizi kutoka Sudan. Alitoa hotuba katika Kiingereza ingawa hakukijua vizuri, na ikatafsiriwa katika Kiarabu. Zekaria hakuwa na hakika iwapo ndugu walielewa hotuba hiyo. Baada ya miaka mitano hivi, vijana wawili waliotembelea Betheli walimjia na kumuuliza: “Je, unatukumbuka? Tulikuwa miongoni mwa watu waliosikiliza hotuba yako katika kambi ya wakimbizi. Tulikumbuka kitia moyo chako, tukaanza kujifunza Biblia.” Baadaye, vijana hao waliweka maisha yao wakfu kwa Yehova.

  • Jamhuri Ya Kidemokrasia Ya Kongo (Kinshasa)
    2004 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehovah
    • [Picha katika ukurasa wa 235]

      Zekaria Belemo atembelea kikundi cha ndugu wakimbizi kutoka Sudan akiwa mwangalizi anayesafiri

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki