-
Jamhuri Ya Kidemokrasia Ya Kongo (Kinshasa)2004 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehovah
-
-
1954: Sosaiti na kazi ya mashahidi wa Yehova ingali imepigwa marufuku kabisa katika Kongo ya Ubelgiji
-
-
Jamhuri Ya Kidemokrasia Ya Kongo (Kinshasa)2004 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehovah
-
-
Utendaji wa Mashahidi wa Yehova na wa Kitawala ulipigwa marufuku.
-
-
Jamhuri Ya Kidemokrasia Ya Kongo (Kinshasa)2004 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehovah
-
-
1955: Bado kazi imepigwa marufuku nchini na haielekei kwamba marufuku itaondolewa karibuni, lakini bidii ya wale wanaompenda na kumtumikia Yehova haijapungua.
-
-
Jamhuri Ya Kidemokrasia Ya Kongo (Kinshasa)2004 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehovah
-
-
Mwezi wa Novemba, Ndugu [Milton G.] Henschel alifika Leopoldville, akakutana moja kwa moja na maofisa wa serikali ya Kongo ya Ubelgiji, akatoa ombi ili marufuku iliyowekewa Sosaiti na Mashahidi wa Yehova ifutiliwe mbali. Alirudi tena Leopoldville na baadaye wawakilishi kutoka New York na Brussels wakaja. Baadaye mtaalamu wa masuala ya Afrika kutoka Ubelgiji alitembelea ofisi ya tawi ya Rhodesia Kaskazini, na ndugu walitumia nafasi hiyo kumweleza kinaganaga kuhusu kazi yetu na ujumbe wetu.
Bado kazi imepigwa marufuku, na akina ndugu katika Kongo ya Ubelgiji wanafanya kazi chini ya hali ngumu sana.
-
-
Jamhuri Ya Kidemokrasia Ya Kongo (Kinshasa)2004 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehovah
-
-
1958: Mwaka uliopita, ujumbe wa Ufalme ulihubiriwa kotekote licha ya kwamba kazi ya kuhubiri habari njema ingali imepigwa marufuku, na ndugu wanafungwa gerezani.
-
-
Jamhuri Ya Kidemokrasia Ya Kongo (Kinshasa)2004 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehovah
-
-
1959: Kwa mara ya kwanza wakuu wa serikali waliwaruhusu akina ndugu wafanye mikutano ya kutaniko, ingawa bado kazi imepigwa marufuku.
-
-
Jamhuri Ya Kidemokrasia Ya Kongo (Kinshasa)2004 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehovah
-
-
Ingawa haikuwezekana bado kuwatuma mishonari nchini Kongo, sheria iliyoidhinisha uhuru wa ibada wa kadiri fulani, ambayo ilitiwa sahihi Juni 10, 1958, iliwaruhusu Mashahidi wa Yehova “kukutana katika nyumba.”
-
-
Jamhuri Ya Kidemokrasia Ya Kongo (Kinshasa)2004 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehovah
-
-
1960: Kazi katika Kongo ya Ubelgiji iliendelea vizuri sana mwaka uliopita. Ndugu wamekuwa wakikutana kwa ukawaida kwenye Majumba ya Ufalme, licha ya kwamba kuna magumu nchini na kazi haijaandikishwa kisheria.
-