-
Jinsi Tulivyoponyoka Mlipuko wa Volkano Wenye Kuogofya!Amkeni!—2002 | Novemba 8
-
-
Msaada Waja Haraka
Mashahidi kutoka Kigali, mji mkuu wa Rwanda, wanajiunga nasi Ijumaa adhuhuri, Januari 18. Halmashauri ya kutoa msaada iliyofanyizwa na ndugu kutoka Goma na Gisenyi inaanza kazi. Jambo la kwanza ni kuwaandalia wakimbizi Mashahidi mahali pa kukaa katika Majumba sita ya Ufalme yaliyo katika eneo hili. Hilo lafanywa siku iyo hiyo. Ishara iliyoandikwa katika Kifaransa na Kiswahili inawekwa kando ya barabara, kuonyesha njia ya kuingia Jumba la Ufalme, ambapo wakimbizi wanaweza kupata msaada na faraja. Pia, siku iyo hiyo, tani tatu za bidhaa za kutosheleza mahitaji ya msingi zawasili katika Majumba ya Ufalme ambapo Mashahidi wanakaa. Siku inayofuata, Jumamosi, lori lililojaa chakula, mablanketi, makaratasi ya plastiki, sabuni, na dawa lawasili kutoka Kigali.
-
-
Jinsi Tulivyoponyoka Mlipuko wa Volkano Wenye Kuogofya!Amkeni!—2002 | Novemba 8
-
-
Hesabu sahihi inaonyesha kwamba familia 180 za Mashahidi ni miongoni mwa zile zilizopoteza kila kitu na hazina mahali pa kuishi. Halmashauri ya kutoa misaada inapanga kuwasaidia wanaume, wanawake, na watoto wapatao 5,000 kupata chakula chao cha kila siku. Plastiki za kutengenezea mahema zilizotolewa na Mashahidi wa Yehova wa Ubelgiji, Ufaransa, na Uswisi zitatumiwa kuunda makao ya muda kwa wale wasio na mahali pa kuishi na vilevile mahali pa kukutana kwa makutaniko ambayo Majumba yao ya Ufalme yaliharibiwa. Baadhi ya jamaa zitaishi pamoja na jamaa nyingine za Mashahidi ambazo nyumba zao hazikuharibiwa, na nyingine zitaishi katika makao hayo ya muda.
Mnamo Ijumaa, Januari 25, siku kumi hivi baada ya usiku wa mlipuko, watu 1,846 wanahudhuria mkutano katika uwanja wa shule huko Goma kusikiliza maneno yenye kutia moyo kutoka kwa Maandiko. Ndugu wengi wanatoa shukrani kwa ajili ya faraja na msaada waliopokea kutoka kwa Yehova kupitia tengenezo lake. Mioyo yetu sisi wageni inaguswa na ujasiri na imani yenye nguvu ya ndugu hao licha ya masaibu yaliyowapata. Katika hali hizo ngumu, ni vyema kama nini kuwa sehemu ya udugu ulioungana katika ibada ya Mungu wa kweli, Yehova, aliye Chanzo cha faraja ya milele!—Zaburi 133:1; 2 Wakorintho 1:3-7.
-