Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Jamhuri Ya Kidemokrasia Ya Kongo (Kinshasa)
    2004 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehovah
    • 1945: Ni mtu jasiri tu anayeweza kumwakilisha Mungu na Ufalme wake katika [Kongo ya Ubelgiji]. Licha ya kwamba kazi na vichapo vimepigwa marufuku kabisa, Wakongomani Waafrika wanaoshirikiana nasi wanaweza kuhamishwa hadi wilaya nyingine na nyakati nyingine wanaishi huko chini ya vizuizi kwa miaka kadhaa. Mara nyingi barua tunazotumiwa kutoka Kongo hazifiki hapa [Rhodesia Kaskazini], na inaonekana kwamba barua tunazotuma hazipelekwi; lakini . . . tunafanya kila tuwezalo kuwasaidia wafanyakazi wenzetu wa Ufalme katika nchi hiyo yenye makasisi chungu nzima.

  • Jamhuri Ya Kidemokrasia Ya Kongo (Kinshasa)
    2004 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehovah
    • Kwa miaka mingi, wahubiri Waafrika wamefungwa gerezani kwa muda usiojulikana kwa sababu ya kazi yao ya kuhubiri, na jambo baya hata zaidi ni kwamba wao hupelekwa kwenye kambi maalumu ya mateso huko Kasaji, kilometa [500] hivi kutoka Elisabethville [sasa ni Lubumbashi]. Wanafanya kazi ngumu kwenye mashamba madogo kambini, na wanatengwa peke yao au pamoja na familia zao. . . . Wengine wao hukaa huko hata kwa miaka kumi. Kwa kawaida, wanakaa peke yao kwa miaka mingi sana bila kutarajia kuwekwa huru au kutendewa haki. Wanaweza kuwekwa huru tu wakifanya uamuzi mbaya wa kukana imani yao.

      Kwa sababu hiyo ndugu wamelazimika kuendelea na kazi yao kisiri; mikutano hufanywa kisiri mahali mbalimbali ili ndugu wasikamatwe. Walihubiri hasa kwa kuwatembelea watu wenye urafiki na marafiki wao, lakini bado mashahidi wengi wametumbukia taabani licha ya tahadhari hizo. Mashahidi hukamatwa na kupelekwa himahima kwenye kambi ya Kasaji.

  • Jamhuri Ya Kidemokrasia Ya Kongo (Kinshasa)
    2004 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehovah
    • 1950: Mwaka uliopita ulikuwa mgumu kuliko miaka mingine yote, na ndugu wanaoishi Kongo ya Ubelgiji waliteseka sana. Mwanzoni mwa mwaka wa utumishi, hawakupokea vitabu wala barua zote zilizotumwa, na karibu mawasiliano na makutaniko yakatizwe kabisa. Kisha, Januari 12, gavana mkuu alipiga marufuku Sosaiti na akatangaza kwamba mtu yeyote atakayehudhuria mkutano, kuunga mkono Sosaiti kwa njia yoyote, au kuwa mfuasi wake, atahukumiwa kifungo cha miezi miwili na kulipa faini ya faranga 2,000. Wachapishaji wa vitabu vya Wakatoliki waliusifu sana uamuzi huo. Ndugu wakaanza kukamatwa. Orodha zilizochukuliwa mwaka uliotangulia kutoka kwa ndugu ambaye awali alikuwa mwangalizi [wa kutaniko] huko Elisabethville, zilitumiwa kuwasaka mamia ya watu walioshirikiana na Sosaiti, nao walikamatwa pamoja na wake zao. Baada ya kukamilisha vifungo vyao, Waafrika wa Rhodesia Kaskazini walifukuzwa nchini, lakini mara nyingi ndugu Wakongomani walipelekwa kwenye kambi ya mateso ya Kasaji, kilometa [500 hivi] kutoka Elisabethville. Ndugu fulani wangali kambini humo. Baadhi ya ndugu waliofukuzwa nchini walipewa chakula kidogo sana, wakalazimishwa kutembea umbali wa kilometa 30 kutoka Sakania hadi kwenye mpaka wa Rhodesia Kaskazini.

      Idadi ya askari wapelelezi imeongezeka karibuni, na mtu yeyote aliye na Biblia anaweza kushukiwa kuwa Shahidi wa Yehova.

      Tumepokea habari kwamba dada wawili Wazungu kutoka wilaya ya Elisabethville wamehukumiwa kifungo cha nje cha siku 45 kwa sababu ya kupatikana na gazeti la Mnara wa Mlinzi na kuhubiri, na watachunguzwa kwa miaka mitatu kuhakikisha kwamba hawahubiri (bila shaka hiyo inamaanisha kwamba hawawezi kufanya kazi ya Bwana). Kila siku dada hao hukabili uwezekano wa kufukuzwa nchini.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki