Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Zambia
    2006 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • Gazeti Times of Zambia linaripoti: “Inafurahisha kwamba shirika la Mashahidi wa Yehova la Zambia limewatuma wafanyakazi wa kujitolea na wa kuandaa msaada katika nchi iliyoitwa Zaire ili kupunguza matatizo ya wakimbizi katika eneo la Maziwa Makuu.” Makala hiyo ilisema kwamba Mashahidi kutoka Ubelgiji, Ufaransa, na Uswisi “waliwapa wakimbizi jumla ya kilo 500 [pauni 1,100] za dawa, tani 10 za bidhaa zenye vitamini, tani 20 za chakula, zaidi ya tani 90 za nguo, njozi 18,500 za viatu, na blanketi 1,000. Gharama ya vitu hivyo ilikuwa dola milioni moja hivi za Marekani.”

  • Zambia
    2006 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • Mashahidi wa Yehova wanajulikana kwa kudumisha amani miongoni mwa wakimbizi. Ofisa fulani wa serikali alisema: “Tulisikia kwamba Mashahidi wa Yehova wanamcha Mungu sana, hivyo tukawaomba baadhi yao wasimamie vikundi mbalimbali kambini. Tangu hapo, kuna utulivu kambini kwa sababu wanatusaidia sana, na kila mtu anajitahidi kusoma Biblia. Ninamshukuru Mungu kwa kuwa na watu kama hao na kwa sababu kuna amani kambini.”

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki