-
Jamhuri Ya Kidemokrasia Ya Kongo (Kinshasa)2004 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehovah
-
-
Hata hivyo, kwa sababu ya watu kuhama kati ya Kongo na Rhodesia Kaskazini, ndugu fulani wa Rhodesia waliweza kuingia Kongo kwa vipindi vifupi.
1945: Ni mtu jasiri tu anayeweza kumwakilisha Mungu na Ufalme wake katika [Kongo ya Ubelgiji]. Licha ya kwamba kazi na vichapo vimepigwa marufuku kabisa, Wakongomani Waafrika wanaoshirikiana nasi wanaweza kuhamishwa hadi wilaya nyingine na nyakati nyingine wanaishi huko chini ya vizuizi kwa miaka kadhaa. Mara nyingi barua tunazotumiwa kutoka Kongo hazifiki hapa [Rhodesia Kaskazini], na inaonekana kwamba barua tunazotuma hazipelekwi; lakini . . . tunafanya kila tuwezalo kuwasaidia wafanyakazi wenzetu wa Ufalme katika nchi hiyo yenye makasisi chungu nzima.
-
-
Jamhuri Ya Kidemokrasia Ya Kongo (Kinshasa)2004 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehovah
-
-
Karibu wakati huo, Llewelyn Phillips, kutoka ofisi ya tawi ya Rhodesia Kaskazini, alienda Kongo ya Ubelgiji ili kuwatetea Mashahidi waliokuwa wakiteswa. Gavana mkuu na maofisa wengine wa serikali walimsikiliza alipokuwa akiwaeleza kuhusu kazi ya kuhubiri ujumbe wa Ufalme na tofauti iliyopo kati ya mafundisho ya Mashahidi na ya Kitawala. Gavana mkuu alimkatiza na kumwuliza hivi huku akiwaza sana: “Nikiwasaidia, itakuwaje kwangu?” Alijua kwamba Kanisa Katoliki lilikuwa na uvutano mkubwa katika nchi hiyo.
1950: Mwaka uliopita ulikuwa mgumu kuliko miaka mingine yote, na ndugu wanaoishi Kongo ya Ubelgiji waliteseka sana. Mwanzoni mwa mwaka wa utumishi, hawakupokea vitabu wala barua zote zilizotumwa, na karibu mawasiliano na makutaniko yakatizwe kabisa.
-