-
Zambia2006 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
-
-
Mnamo Februari 3, 1962, ofisi mpya ya tawi, iliyokuwa na makao, chumba cha uchapaji, na Jumba la Ufalme, iliwekwa wakfu kwa Yehova.
-
-
Zambia2006 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
-
-
Ian Fergusson alisema: “Ndugu Knorr alituhimiza tupanue kiwanda chetu cha uchapaji. Nilitembelea ofisi ya tawi ya Elandsfontein, Afrika Kusini, ili kushauriana na akina ndugu. Muda mfupi baadaye, mashine ya kuchapa ikasafirishwa kwa ndege hadi Kitwe.”
Huduma Yetu ya Ufalme ya kila mwezi na pia magazeti na vichapo vingine kwa ajili ya Kenya na nchi nyingine za Afrika Mashariki, vilikuwa vikichapwa huko Kitwe. Punde baadaye, kiwanda chetu cha uchapaji kikawa kidogo sana na ikatubidi kujenga kiwanda kipya. Baraza la mji lilipotuzuia tusijenge kiwanda hicho katika kiwanja fulani kilichokuwa kimepatikana, ndugu mmoja alitupa kiwanja. Ujenzi ulikamilika katika 1984.
-