-
Ujenzi wa Kiroho Katika “Nyumba ya Mawe”Mnara wa Mlinzi—2007 | Februari 15
-
-
KWA nini iliitwa Nyumba ya Mawe? Mnamo 1867, Adam Renders, ambaye alikuwa mwindaji na mvumbuzi, aliona magofu makubwa ya mawe katika eneo lenye ukubwa wa ekari 1,800. Alikuwa akisafiri kwenye mbuga za Afrika ambako kwa kawaida nyumba zilijengwa kwa udongo, miti, na kuezekwa nyasi. Kisha, akafika kwenye magofu ya mawe ya jiji kubwa, ambalo sasa linaitwa Great Zimbabwe.
Magofu hayo yako kusini mwa eneo ambalo sasa linaitwa Masvingo. Kuta nyingine zina kimo cha mita 9, na mawe ya matale yamepangwa moja juu ya lingine bila kushikanishwa na sementi. Katika magofu hayo, kuna mnara wa pekee wenye umbo la pia unaofikia mita 11 hivi kutoka kwenye jukwaa la mviringo lenye kipenyo cha mita 6. Kusudi la jengo hilo bado halijulikani. Magofu yake ni ya karne ya nane W.K., lakini kuna uthibitisho wa kwamba eneo hilo lilikaliwa mamia ya miaka kabla ya wakati huo.
-
-
Ujenzi wa Kiroho Katika “Nyumba ya Mawe”Mnara wa Mlinzi—2007 | Februari 15
-
-
[Picha katika ukurasa wa 9]
Mnara wenye umbo la pia
-
-
Ujenzi wa Kiroho Katika “Nyumba ya Mawe”Mnara wa Mlinzi—2007 | Februari 15
-
-
[Hisani ya Picha katika ukurasa wa 9]
Ruins with steps: ©Chris van der Merwe/AAI Fotostock/age fotostock; tower inset: ©Ingrid van den Berg/AAI Fotostock/age fotostock
-