-
Kulea Watoto Afrika Wakati wa MagumuAmkeni!—1999 | Oktoba 22
-
-
Bertie alipoachiliwa kutoka gerezani, tuliamua kuhamia Bulawayo, kwa kuwa migodi haikuwa ikiendelea vizuri. Bertie alipata kazi kwenye reli, nami niliongezea mapato yetu kwa kutumia stadi zangu mpya nilizopata nikiwa mshonaji.
Kazi ya Bertie akiwa mpiga-ribiti kwenye reli ilionekana kuwa ya muhimu, kwa hiyo akaepushwa na utumishi wa kijeshi.
-
-
Kulea Watoto Afrika Wakati wa MagumuAmkeni!—1999 | Oktoba 22
-
-
Baada ya vita Bertie aliomba shirika la reli limhamishe hadi Umtali (ambayo sasa ni Mutare), mji wenye kupendeza mpakani mwa Msumbiji. Tulitaka kutumikia mahali palipo na uhitaji mkubwa zaidi wa wahubiri wa Ufalme, na Umtali palionekana kuwa mahali pafaapo, kwa kuwa jiji hilo halikuwa na Mashahidi. Katika kipindi hicho kifupi tulichokaa huko, familia ya Holtshauzen, ambayo ilitia ndani wana watano, ikawa Mashahidi. Sasa kuna makutaniko 13 katika jiji hilo!
Mwaka wa 1947 familia yetu ilizungumzia uwezekano wa Bertie kurudia kazi ya upainia. Lyall, ambaye alikuwa amerudi kutoka kupainia kule Afrika Kusini, aliunga mkono wazo hilo. Donovan alikuwa akipainia Afrika Kusini wakati huo. Wakati ofisi ya tawi ya Cape Town ilijua tamaa ya Bertie ya kupainia tena, walimwomba afungue depo ya vichapo huko Bulawayo badala yake. Kwa hiyo alistaafu kutoka shirika la reli, na tukahamia huko.
-
-
Kulea Watoto Afrika Wakati wa MagumuAmkeni!—1999 | Oktoba 22
-
-
Twahamia Rhodesia Kusini
Hatimaye, kaka ya Bertie, Jack, alitualika tujiunge naye katika kazi hatari ya migodi ya dhahabu karibu na Filabusi, huko Rhodesia Kusini. Mimi na Bertie tulisafiri huko pamoja na Peter, wakati huo akiwa na umri wa mwaka mmoja, huku mama yangu akitunza Lyall na Donovan kwa muda.
-
-
Kulea Watoto Afrika Wakati wa MagumuAmkeni!—1999 | Oktoba 22
-
-
Mimi na Bertie Twatiwa Gerezani
Tulisafiri hadi jiji la Bulawayo mara moja kwa mwezi, umbali wa kilometa 80 hivi, kuuza dhahabu yetu katika benki. Pia tulikwenda Gwanda, mji mdogo karibu na Filabusi, kununua vyakula na kushiriki katika huduma. Katika 1940, mwaka ambao Vita ya Ulimwengu ya Pili ilianza, kazi yetu ya kuhubiri ilipigwa marufuku katika Rhodesia Kusini.
Muda mfupi baada ya hapo, nilikamatwa nikihubiri huko Gwanda. Wakati huo nilikuwa na mimba ya mtoto wangu wa tatu, Estrella. Wakati rufani yangu ilipokuwa ikifikiriwa, Bertie alikamatwa kwa sababu ya kuhubiri na kutiwa gerezani katika Salisbury, zaidi ya kilometa 300 kutoka mahali tulipokuwa tukiishi.
-
-
Kulea Watoto Afrika Wakati wa MagumuAmkeni!—1999 | Oktoba 22
-
-
Kisha mwaka 1950, ofisi ya tawi ilihamishwa hadi Salisbury, jiji kuu la Rhodesia Kusini, nasi tukahamia kule pia. Tulinunua nyumba kubwa mno ambamo tuliishi kwa miaka mingi. Sikuzote mapainia na wageni walitutembelea na kukaa nasi, kwa hiyo mahali petu pakajulikana kuwa hoteli ya McLuckie!
Mwaka wa 1953, mimi na Bertie tulihudhuria mkusanyiko wa kimataifa wa Mashahidi wa Yehova katika Yankee Stadium huko New York City. Hilo lilikuwa tukio lisilosahaulika kama nini! Miaka mitano baadaye, Lyall, Estrella, Lindsay, na Jeremy mwenye umri wa miezi 16 walikuwa pamoja nasi kwenye mkusanyiko huo wa kimataifa mkubwa mno wa siku nane mwaka wa 1958 katika Yankee Stadium na Polo Grounds iliyo karibu na hapo.
-
-
Kulea Watoto Afrika Wakati wa MagumuAmkeni!—1999 | Oktoba 22
-
-
Bertie alitumikia kwa miaka 14 akiwa mfanyakazi mwenye kusafiri kila siku kwenye ofisi ya tawi ya Salisbury, lakini tukaamua kutumikia mahali penye uhitaji mkubwa zaidi huko Shelisheli.
-
-
Kulea Watoto Afrika Wakati wa MagumuAmkeni!—1999 | Oktoba 22
-
-
Safari ya Kurudi Yenye Hatari Sana
Tulipofika Mombasa, tulichukua gari letu na kuelekea kusini kupitia barabara ya pwani yenye changarawe. Tulipofika Tanga, injini ya gari letu ilizima. Fedha zetu zilikuwa karibu kwisha, lakini mtu wa jamaa na Shahidi mwingine walitusaidia. Tulipokuwa Mombasa, ndugu mmoja alijitolea kutusaidia kifedha kama tungeenda kaskazini hadi Somalia kuhubiri. Hata hivyo, sikuwa mzima, kwa hiyo, tulitaka tu kurudi nyumbani Rhodesia Kusini.
Tulivuka kutoka Tanganyika hadi Nyasaland na kusafiri hadi upande wa magharibi wa Ziwa Nyasa, sasa liitwalo Ziwa Malawi. Nilikuwa mgonjwa sana hivi kwamba nikamwomba Bertie aniweke kandokando ya barabara nife! Tulikuwa karibu na jiji la Lilongwe, kwa hiyo alinipeleka hospitalini huko. Sindano za afyuni zilinipa kitulizo kidogo. Kwa kuwa sikuweza kuendelea na safari kwa gari, Bertie na watoto waliendesha gari kilometa 400 hivi hadi Blantyre. Mtu fulani wa jamaa alipanga nisafiri kwa ndege siku chache baadaye ili nijiunge nao. Kutoka Blantyre nilisafiri kwa ndege kurudi Salisbury, na Bertie na watoto walisafiri kwenda nyumbani kwa gari.
Sisi sote tulifurahi kama nini kufika Salisbury nyumbani kwa binti yetu Pauline na mume wake! Mwaka wa 1963 mwana wetu wa mwisho, Andrew, alizaliwa. Alikuwa na tatizo la pafu naye hakutazamiwa kuishi, lakini kwa tokeo zuri akaishi.
-