-
Chui wa Ajabu wa ThelujiAmkeni!—2002 | Mei 8
-
-
Chui wa Theluji Katika Bustani ya Wanyama ya Helsinki
Bustani ya Wanyama ya Helsinki imefanikiwa sana kuzalisha chui wa theluji. Mnamo 1976 bustani hiyo ilipewa jukumu la kuweka rekodi za chui wa theluji ulimwenguni kote. Rekodi hiyo imekuwa muhimu katika kushughulikia chui wa theluji wanaohifadhiwa.
Kuna rekodi nyingine kama hizo za aina nyingi za wanyama wanaohifadhiwa katika bustani za wanyama, lakini hasa ni za wale walio karibu kutoweka. Rekodi hizo huorodhesha habari za wanyama wote wa aina moja wanaoishi katika bustani ya wanyama. Bustani za wanyama zina jukumu la kutoa habari kwa mweka-rekodi kuhusu wanyama wanaozaliwa na pia wale wanaohamishwa au kufa. Rekodi hizo hutumiwa kuchagua wanyama watakaotumiwa kuzalisha wanyama wengine. Blomqvist anaeleza: “Kwa kuwa wanyama si wengi, ubora wa wanyama wanaozaliwa unaweza kupungua kwa urahisi kwa sababu ya kuzaana kati yao tu.”
Zaidi ya chui wachanga mia moja wamezaliwa katika Bustani ya Wanyama ya Helsinki pekee, na wengi wao wamehamishwa hadi kwenye bustani nyingine za wanyama. Ili kuhakikisha kuna namna nyingi za chui wa theluji, wanyama hubadilishwa kutoka kwenye bustani moja ya wanyama hadi nyingine. Sasa kuna namna nyingi za chui wa theluji katika bustani za wanyama hivi kwamba hakuna haja tena ya kuwashika wale walioko mwituni.
Bustani nyingi za wanyama, kutia ndani ile ya Helsinki, zinasaidia kuhifadhi wanyama-pori wenye afya. Bila shaka, bustani hizo pia husaidia wale wanaozitembelea kuona wanyama wa kipekee. Kwa kweli, yule ambaye amemwona chui wa theluji hawezi kumsahau kwa urahisi na sifa zinamwendea Muumba ambaye ‘amefanya kila kitu kizuri.’—Mhubiri 3:11.
-
-
Chui wa Ajabu wa ThelujiAmkeni!—2002 | Mei 8
-
-
Chui wa Ajabu wa Theluji
NA MWANDISHI WA AMKENI! NCHINI FINLAND
SI WANYAMA wengi walio wa ajabu kama chui wa theluji. Ni watu wachache tu ambao wamemwona mwituni, si mengi yanayojulikana kuhusu maisha yake.
Chui wa theluji anavutia watu wengi katika Bustani ya Wanyama ya Helsinki, nchini Finland. Anavutia sana kwa tabia zake za ajabu, na hata wengi humwona kuwa mrembo zaidi katika familia ya wanyama ya paka wakubwa.
-
-
Chui wa Ajabu wa ThelujiAmkeni!—2002 | Mei 8
-
-
Kulingana na Leif Blomqvist, msimamizi wa Bustani ya Wanyama ya Helsinki, “chui wa theluji ni mpole sana. Yeye hufanya urafiki na wanadamu kwa urahisi, na yeye huja asubuhi kwenye bustani ya wanyama kumsalimia yule anayemhudumia.” Blomqvist anaongeza kusema kwamba chui wadogo wa theluji ni wapole pia. Anasema hivi: “Wao hawang’ang’ani na wafanyakazi wakati wanapopimwa au kupewa chanjo.” Lakini namna gani ukimshika chui wa aina nyingine wa umri huo? “Ni vigumu sana kuwashika,” Blomqvist anasema. “Unahitaji mavazi na glavu za kujikinga, kwa sababu wao wanaweza kumshambulia mtu.”
-