-
Kuchunguza Bustani za Kisasa za WanyamaAmkeni!—2012 | Septemba
-
-
Katika kujibu madai hayo, watu wanaotunza bustani za wanyama wanasema kwamba bustani hizo zinatimiza fungu muhimu katika kuwahifadhi wanyama na kuwaelimisha watu. “Lengo letu ni kuwafundisha watu jinsi ya kuwaheshimu wanyama,” anaeleza Jaime Rull, kutoka Bustani ya Faunia, Madrid, Hispania. “Tunataka kuwachochea wageni wanaotembelea bustani yetu wawe na tamaa ya kutunza mazingira ya wanyama kwani watatoweka maeneo hayo yasipotunzwa.” Utafiti fulani unaonyesha kwamba bustani nyingi zimefanikiwa kuwahamasisha watu waone uhitaji wa kulinda wanyama wanaokabili hatari ya kutoweka.
Inaonekana kwamba baadhi ya aina za wanyama wanaokabili hatari ya kutoweka kama vile panda mkubwa wanapendwa sana na watu. “Watu wote wanaotembelea hapa wanataka kuwaona panda wetu wawili,” anasema Noelia Benito, wa Hifadhi ya Wanyama ya Madrid. “Wanyama hao maarufu wamekuwa kama alama ya mapambano yetu ya kuhifadhi wanyama wanaokabili hatari ya kutoweka. Tunatumaini kwamba panda hao watazaana, ingawa panda hawakubali kuzaa na panda yeyote tu.”
Tofauti na panda, wanyama wengine huzaana kwa urahisi katika bustani za wanyama kwa sababu ya mazingira yaliyoboreshwa na matibabu wanayopata. Kwa kuwa wanyama wengi wamefanikiwa kuzaana katika bustani hizo, hilo limesaidia kujibu maswali ya wachambuzi wanaosema kwamba bustani hizo hazipaswi kujihusisha katika biashara ya kununua au kuuza wanyama wanaokabili hatari ya kutoweka kutoka katika mazingira yao ya asili. Zaidi ya kuhakikisha kwamba kuna wanyama katika bustani yao, bustani nyingi hujaribu kuzalisha wanyama wanaokabili hatari ya kutoweka wakiwa na lengo la kuwarudisha katika mazingira yao ya asili.
Chanzo kikuu cha kutoweka kwa wanyama ni kupotea kwa makao yao ya asili. Kwa hiyo, bustani za wanyama zimejihusisha sana katika kufadhili programu za kuhifadhi mazingira, zikishirikiana kwa ukaribu na hifadhi za wanyama-pori katika nchi zenye joto.a
-
-
Kuchunguza Bustani za Kisasa za WanyamaAmkeni!—2012 | Septemba
-
-
a Inaonekana kwamba jitihada zinazofanywa na bustani za wanyama kuwalinda simbamarara huko Asia, komba wa Madagaska, na nyani wa Afrika zimefanikiwa.
-