-
Aliilinda Familia Yake, Akawaandalia, na AkavumiliaMnara wa Mlinzi—2012 | Aprili 1
-
-
YOSEFU aliweka mzigo mwingine kwenye mgongo wa punda. Wazia akitazama huku na huku kwenye kijiji cha Bethlehemu wakati wa usiku na kumpigapiga ubavuni mwana-punda huyo mwenye nguvu. Bila shaka, alikuwa akifikiria safari ndefu iliyokuwa mbele yao. Misri! Watu wa nchi nyingine, lugha tofauti, tamaduni za kigeni—familia yake ndogo ingekabilianaje na mabadiliko hayo yote?
Haikuwa rahisi kwa Yosefu kumwambia Maria, mke wake mpendwa, habari hizo mbaya. Hata hivyo, alijikaza na kumwambia. Alimwambia kuhusu ndoto aliyoota ambapo malaika alimpa ujumbe huu kutoka kwa Mungu: Mfalme, Herode, alitaka kumuua mwana wao mchanga! Walipaswa kuondoka mara moja. (Mathayo 2:13, 14) Jambo hilo lilimhangaisha sana Maria. Kwa nini mtu fulani alitaka kumuua mtoto wake asiye na hatia? Maria na Yosefu hawakuelewa jambo hilo. Lakini waliamini jambo ambalo Yehova alisema, hivyo wakajitayarisha.
Huku watu katika kijiji cha Bethlehemu wakiwa wamelala, bila kujua kilichokuwa kikiendelea, Yosefu, Maria, na Yesu wakaondoka kimyakimya usiku. Yosefu alipoiongoza familia yake upande wa kusini huku mwangaza ukianza kuonekana upande wa mashariki, inaelekea alijiuliza jinsi ambavyo hali ingekuwa baadaye. Seremala wa hali ya chini angewezaje kuilinda familia yake kutokana na watu wenye nguvu nyingi? Je, angefaulu kuiandalia familia yake sikuzote? Je, angefanikiwa kutimiza kwa uvumilivu mgawo mzito ambao Yehova Mungu alikuwa amempa, mgawo wa kumlinda na kumlea mtoto huyo wa pekee? Yosefu alikabili hali nyingi ngumu.
-
-
Aliilinda Familia Yake, Akawaandalia, na AkavumiliaMnara wa Mlinzi—2012 | Aprili 1
-
-
Muda mfupi baada ya wanajimu hao kuondoka, Yosefu alipewa onyo hili na malaika wa Yehova: “Simama, mchukue huyo mtoto mchanga na mama yake mkimbie kuingia Misri, mkae huko mpaka nikupe agizo; kwa maana Herode yuko karibu kumtafuta huyo mtoto amwangamize.” (Mathayo 2:13) Kwa hiyo, kama tulivyoona mwanzoni, Yosefu alitii bila kusita. Alitanguliza kabisa usalama wa mtoto wake na akaondoka na familia yake kwenda Misri. Kwa kuwa wale wanajimu wapagani waliipa familia hiyo vitu vyenye thamani, sasa walikuwa na vitu ambavyo vingewasaidia katika safari iliyokuwa mbele yao.
Baadaye, mafumbo ya apokrifa na hekaya nyingine zilitia chumvi safari hiyo ya kwenda Misri, na kudai kwamba mtoto Yesu alifupisha safari hiyo kimuujiza, akawashinda nguvu majambazi, na hata akafanya mitende iiname ili mama yake achume matunda yake.c Ukweli ni kwamba walitembea mwendo mrefu wenye kuchosha bila kujua waendako.
-
-
Aliilinda Familia Yake, Akawaandalia, na AkavumiliaMnara wa Mlinzi—2012 | Aprili 1
-
-
c Biblia inaonyesha waziwazi kwamba Yesu alifanya muujiza wake wa kwanza baada ya kubatizwa. (Yohana 2:1-11) Kwa habari zaidi kuhusu masimulizi ya injili za apokrifa, ona makala “Injili za Apokrifa—Je, Zina Ukweli Uliofichwa Kumhusu Yesu?” kwenye ukurasa wa 18.
-