-
RSD—Ugonjwa wa Kukoroweza na Wenye MaumivuAmkeni!—1997 | Septemba 8
-
-
Madhara yasiyoweza kurekebishwa yaweza kuzuiwa, kulingana na Dakt. Howard Intrater, mkurugenzi wa kliniki ya maumivu katika Health Sciences Centre huko Winnipeg. Mfumo wa neva uitwao sympathetic nervous system, wapasa kuzuiwa ili usitume ishara za maumivu.a Gazeti la habari la Winnipeg laripoti kwamba “matibabu hutofautiana kutoka kichocheo cha umeme hadi dawa za beta blockers, kichocheo cha epidural (ambapo elektrodi inawekwa katika uti wa mgongo ili kuamsha eneo lililoathirika hadi kuzuia sympathetic nerve kwa kutumia sindano.” Tibamaungo inatumiwa pamoja na tiba ya vitobo ili kupunguza maumivu na kuongeza uwezo wa kujongea. Jarida British Medical Journal lasema kwamba “matibabu yenye matokeo yatia ndani baadhi ya mchanganyiko wa kusisimua neva kwa umeme, kuzuia sympathetic nerve kwa kemikali, tiba ya kisaikolojia, na tiba ya mazoezi yenye juhudi nyingi ya kimwili.”
-
-
Jitihada Yangu ya Kukabiliana na RSDAmkeni!—1997 | Septemba 8
-
-
Kitulizo Fulani Hatimaye!
Hatimaye, ikiwa jitihada ya mwisho, nilipelekwa katika kliniki ya maumivu ili kupata matibabu. Hapo nilikutana na Dakt. Mathew Lefkowitz, ambaye ni mtaalamu wa maumivu aliye pia mtaalamu wa nusukaputi ambaye afanya kazi New York, katika Brooklyn Heights. Alikuwa mwenye huruma sana na mwenye kuelewa. Hiyo kliniki ya maumivu ikawa kimbilio kwangu, hasa nilipoanza kuelewa ugonjwa wangu na matibabu.
Dakt. Lefkowitz alianza na matibabu ya kuondoa maumivu—kudungwa sindano kwa ukawaida katika neva shingoni mwangu, ambazo zingezuia kwa muda ujumbe wa neva unaosababisha maumivu. Kulingana na maelezo yake, maumivu yanasababishwa na sympathetic nervous system. Hili ni itikio la kawaida la ubongo kwa jeraha au upasuaji. Nadharia ni kwamba mfumo huu unapaswa kufanya kazi kama lango. Hisi za neva hupita tu jeraha linapopona. Wakati fulani, ubongo usipoendelea kutuma mipwito ya neva, lango hilo hujifunga na maumivu hupotea. Katika RSD, lango hilo halifungiki. Hiyo sympathetic nervous system haitulii kamwe. Huendelea kufanya kazi kana kwamba bado kuna jeraha katika sehemu hiyo ya mwili. Huyo daktari aliniambia niende katika kliniki hiyo mara moja wakati wowote maumivu yaongezekapo. Hivyo, nimekuwa nikienda kwa ukawaida kwa ajili ya sindano za kuzuia maumivu kwa muda fulani.
Sindano hizo zilinisaidia kuvumilia matibabu ya kuzoeza mwili, ambayo huniwezesha kujongea kiungo kilichoathirika na ni yenye kufaa sana kwa ugonjwa huu wa RSD. Wakati ulipoendelea kupita, nilianza kufanya kazi ndogo-ndogo, nikitumia mikono yote miwili. Ulikuwa mwanzo mzuri.
-
-
Jitihada Yangu ya Kukabiliana na RSDAmkeni!—1997 | Septemba 8
-
-
Maoni ya Daktari
Amkeni! lilimhoji Dakt. Lefkowitz ili kupata maelezo yake juu ya matibabu hayo. Alieleza: “Tunashughulikia maumivu ya aina zote, si RSD pekee. Maumivu ya kawaida sana ni maumivu ya sehemu ya chini ya mgongo, ambayo mara nyingi huongoza katika maumivu makali ya nyonga. Ingawa kwa wazi maumivu ni ya kimwili kwa asili, lakini pia upo uvutano wa kisaikolojia.”
Amkeni!: Je, RSD waweza kushambulia watu wa umri wowote na wa jinsia tofauti bila kubagua?
Dakt. Lefkowitz: Ndiyo, ugonjwa huu haubagui. Hata hivyo, hatuwezi kutabiri ni nani ana mwelekeo zaidi wa kushambuliwa na ugonjwa huu. Kile ninachojua ni kwamba kwa kawaida wanawake huvumilia maumivu zaidi ya wanaume. Wanaonekana wana uwezo zaidi wa kuvumilia maumivu.
Amkeni!: Unapendekeza matibabu gani kwa ajili ya maumivu?
Dakt. Lefkowitz: Kuna njia mbalimbali tuwezazo kutumia, ikitegemea chanzo na kiasi cha maumivu. Kwa vyovyote, maumivu humaanisha kuteseka, na twapaswa kuondoa mateso hayo. Katika visa fulani twatumia vidonge visivyo na steroid, kama vile aspirini, na aina zake nyingine. Katika visa vingine, kama kile cha Karen, twatumia dawa za kuzuia neva mahali penye maumivu. Katika visa vya kupita kiasi twaweza kutumia dawa za kutia usingizi. Tatizo la kutumia dawa ya kutia usingizi ni kwamba twapaswa kuwa waangalifu kwa uwezekano wa uraibu.
Amkeni!: Je, ni lazima RSD upitie hatua zote unapoendelea?
Dakt. Lefkowitz: Hapana, si hivyo. Ikiwa twaweza kugundua ugonjwa huo ukiwa katika hatua ya mwanzo, twaweza kuzuia maendeleo yake. Chukua Karen kama kielelezo. Yupo katika hatua ya katikati, na si lazima aendelee hadi hatua ya mwisho ya kudhoofika kwa kiungo.
Amkeni!: Unapendekeza nini ili kumsaidia mgonjwa kukabiliana na hali hii?
Dakt. Lefkowitz: Vile tu Karen alivyofanya. Amekabili maumivu yake kisaikolojia kwa kukengeusha mawazo yake kwa mawazo mazuri na picha nzuri. Pia atumia matibabu ya kuzoeza mwili. Na ninaamini kwamba imani yake imekuwa msaada mkubwa sana. Imemsaidia kuona hali hiyo kwa njia ifaayo. Ndiyo, siwezi kukazia imani sana.
Amkeni!: Asante sana kwa wakati wako na subira.
-