Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Vito vya Kingo za Mto
    Amkeni!—1997 | Juni 22
    • Mruko wa Kereng’ende

      Kwa kweli kuita kereng’ende helikopta—jina la kubandika la kawaida nchini Hispania—ni ulinganifu wenye kumshusha hadhi kabisa. Sarakasi zao za angani ni za kasi sana hivi kwamba nyakati nyingine haiwezekani kuwafuata kwa macho. Kwa miendo mifupi ya kasi, spishi fulani zaweza kufikia mwendo wa kilometa 96 hivi kwa saa. Wao pia waweza kusimama hewani au kwenda kinyumenyume, mbele au kandokando kwa ghafula. Isitoshe, kereng’ende apigapo kona kali hewani, wanasayansi hukadiria kwamba ni lazima astahimili nguvu za karibu G 2.5.

      Kereng’ende wana mabawa mawili yenye kupindika na yaliyo mepesi. Ingawa mabawa hayo huonekana kuwa dhaifu, hayo yaweza kupiga mara 40 kwa sekunde moja nayo huweza kustahimili kugongwagongwa bila kupatwa na madhara. Mwanabiolojia Robin J. Wootton ayafafanua kuwa “maajabu madogo ya ubuni wenye ustadi.”

      “Kadiri tuelewavyo zaidi kazi ya mabawa ya mdudu,” yeye aongezea, “ndivyo ubuni wayo na umaridadi wa uumbaji wayo uzidivyo kuonekana. . . . Mabawa ya wadudu hayana kifani katika tekinolojia.” Haishangazi kwamba mbinu za mruko wa kereng’ende zinachunguzwa sasa na wahandisi wa ndege.

  • Vito vya Kingo za Mto
    Amkeni!—1997 | Juni 22
    • Uthibitisho Dhidi ya Mageuzi

      Wanasayansi wengi wa mageuzi humfikiria kereng’ende kuwa mdudu wa kuruka wa mapema zaidi kati ya wadudu. Kisukuku kimoja kilichovumbuliwa nchini Ufaransa kilitokeza kwenye miamba kereng’ende fulani mwenye mabawa yenye upana wa sentimeta 75! Ndiye mdudu mkubwa zaidi ajulikanaye, akiwa mkubwa zaidi ya mara tatu kuliko kereng’ende yeyote aishiye.

      ‘Ingewezekanaje,’ nikajiuliza, ‘kwa muundo ulio tata zaidi wa mruko ujulikanao kwa binadamu kutokea tu wenyewe, ukiwa kamili kabisa?’ “Hakuna visukuku vya wadudu ambavyo viko kati ya wenye mabawa na wasio na mabawa,” chakiri kitabu Alien Empire—An Exploration of the Lives of Insects. Ni wazi kwamba kereng’ende ni kazi ya Mbuni Stadi mwenye akili.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki