-
Vipepeo, Mimea na Siafu Wenye Uhusiano MuhimuAmkeni!—2001 | Mei 22
-
-
KATIKA mwezi wa Julai, vipepeo wenye kuvutia wa Ulaya Magharibi hujua kwamba ni wakati wa kuzaa kizazi kipya cha vipepeo. Ili kutokeza kizazi kipya, vipepeo hao wanahitaji mambo mengi mbali na wenzi. Wanahitaji pia maua yenye rangi ya samawati yanayomea eneo lenye majimaji na siafu wekundu wenye njaa. Kwa nini? Mimea na siafu wanahusikaje katika maisha ya vipepeo hao?
Unaweza kuchunguza uhusiano huo wenye kupendeza wa vitu hivyo vitatu katika Mbuga ya Taifa ya Dwingelderveld iliyoko sehemu ya kaskazini mwa Uholanzi. Katika mbuga hiyo kuna vipepeo hao wengi wa rangi ya samawati. Katika majira ya kuchipua na ya kiangazi maua mengi yenye rangi mbalimbali humea katika mbuga ya Dwingelderveld. Kuna maua ya samawati ya eneo lenye majimaji (gentiani), maua ya mbugani nyekundu hafifu, na maua aina ya yungiyungi ya manjano. Vipepeo hao wa samawati wanapenda hasa maua madogo ya mbugani yenye kuvutia na maua ya samawati ya eneo lenye majimaji. Lakini wanayapenda kwa sababu mbili tofauti. Maua ya mbugani yana umajimaji mtamu mwingi ambao vipepeo wanapenda, na maua ya eneo la majimaji ni mahali pazuri pa kuhifadhia vitu.
-
-
Vipepeo, Mimea na Siafu Wenye Uhusiano MuhimuAmkeni!—2001 | Mei 22
-
-
Ili Mbuga ya Taifa ya Dwingelderveld idumu kuwa makao salama ya kipepeo wa samawati, watunzaji wanajaribu kuihifadhi mbuga hiyo kwa kuchunga mifugo hapo jinsi wafugaji walivyofanya mamia ya miaka iliyopita. Kama zamani za kale, wachungaji wanachunga makundi ya kondoo mbugani, na ng’ombe wanalisha kwenye makonde yenye nyasi ngumu. Ng’ombe na kondoo wanapolisha wanaondoa mimea fulani na kwa njia hiyo mimea mbalimbali ya mbugani inaweza kumea vizuri. (Kwa sasa, kuna jamii 580 za mimea katika mbuga hiyo.) Na kwa sababu hiyo vipepeo wa samawati wa Dwingelderveld wanaongezeka idadi. Mbuga hiyo kubwa ni muhimu kuliko mbuga zote za Ulaya, ni makao mazuri sana kwa vipepeo wote hivi kwamba asilimia 60 ya vipepeo wote wa Uholanzi wanapatikana huko.
-