-
Maporomoko ya Maji ya Murchison Nchini UgandaAmkeni!—2011 | Septemba
-
-
Maporomoko ya Maji ya Murchison ni mojawapo ya sehemu zenye kuvutia za eneo lenye ukubwa wa kilomita 3,841 za mraba linalofanyiza Mbuga ya Taifa ya Maporomoko ya Maji ya Murchison. Mbuga hiyo ambayo iko kaskazini magharibi mwa Uganda ilianzishwa mwaka wa 1952.
-
-
Maporomoko ya Maji ya Murchison Nchini UgandaAmkeni!—2011 | Septemba
-
-
[Sanduku/Picha katika ukurasa wa 17]
Mbuga ya Taifa ya Maporomoko ya Maji ya Murchison
Hesabu iliyochukuliwa mwaka wa 1969 ilionyesha kwamba kulikuwa na viboko 14,000 hivi, tembo 14,500, na nyati 26,500 katika mbuga hiyo. Lakini katika makumi ya miaka iliyofuata, idadi ya wanyama hao ilianza kupungua sana. Hivi karibuni, kwa sababu ya jitihada zilizofanywa za kuwalinda wanyama hao, idadi yao imeanza kuongezeka. Sasa, kwenye msitu wa mbuga hiyo kuna aina nyingi za nyani kama vile sokwe-mtu, na katika maeneo tambarare yenye malisho kuna twiga na kongoni wanaoitwa Jackson. Zaidi ya spishi 70 za mamalia na zaidi ya spishi 450 za ndege zimegunduliwa katika mbuga hiyo.
-