-
Puerto Riko—Nchi Yenye UtajiriAmkeni!—2008 | Oktoba
-
-
Hifadhi ya Guánica. Huenda ni asilimia 1 tu hivi ya misitu isiyo na mvua nyingi ambayo bado ipo ulimwenguni. Mojawapo ya misitu hiyo inapatikana mwendo wa saa chache tu kutoka El Yunque. Wataalamu fulani wa mimea wanasema kwamba huenda Guánica “ndio mfano bora wa msitu usio na mvua nyingi ulimwenguni.” Msitu huo ni makao ya ndege wengi wa asili wa Puerto Riko kutia ndani jamii 750 za mimea, na asilimia 7 ya mimea hiyo imo katika hatari ya kutoweka. Maua yake yasiyo ya kawaida huwavutia ndege wavumaji na vipepeo wengi. Kando ya msitu huo kuna fuo safi ambapo kasa wa rangi ya kijani kibichi na wale wenye ngozi laini mgongoni huja kutaga mayai.
Mikoko na Matumbawe. Hifadhi ya Guánica ina msitu wa mikoko kwenye eneo la pwani. “Hifadhi yetu inasaidia mikoko isitawi, kwani hakuna uchafuzi wa kemikali kutoka viwandani na mashambani,” anaeleza mlinzi mmoja wa msitu. “Mikoko hiyo inaandaa mahali pazuri pa kutaga mayai kwa samaki wanaoishi katika matumbawe.” Jambo lingine linalowavutia watalii ni ghuba zinazong’aa zinazotegemea mikoko, na baadhi ya ghuba hizo zinaweza kupatikana huko Puerto Riko.—Ona sanduku hapo chini.
Matumbawe yaliyo karibu na fuo hayajaathiriwa na uvuvi, na visiwa vidogo na matumbawe fulani chini ya bahari yamehifadhiwa kuwa mbuga za taifa. Bustani hizo zilizo chini ya bahari ni sehemu zinazofurahisha wapiga-mbizi ambao wanakutana ana kwa ana na kasa na nguva na pia samaki wengi wenye rangi mbalimbali.
-
-
Puerto Riko—Nchi Yenye UtajiriAmkeni!—2008 | Oktoba
-
-
[Picha katika ukurasa wa 16, 17]
Pwani ya Guánica
[Hisani]
© Heeb Christian/age fotostock
-