-
Kuwahubiria Mbilikimo Kweli za BibliaAmkeni!—2004 | Agosti 22
-
-
Katika nyakati za kisasa, Mashahidi wa Yehova wamekuwa wakihubiri katika misitu ya Afrika. Ingawa Mbilikimo wamekubali ujumbe wa Ufalme, jitihada za kuwarudia hazijafanikiwa sana. Hiyo ni kwa sababu Mbilikimo hupenda kuhamahama kutoka sehemu moja hadi nyingine baada ya miezi kadhaa.
-
-
Kuwahubiria Mbilikimo Kweli za BibliaAmkeni!—2004 | Agosti 22
-
-
Janvier Mbaki ametofautiana sana na wenzake kwani ndiye Mbilikimo wa kwanza kuripotiwa kuwa Shahidi nchini Kamerun. Alikubali ujumbe wa Biblia baada ya kusoma kitabu chenye picha kinachoitwa Unaweza Kuishi Milele Katika Paradiso Duniani, na vitabu vingine.a Janvier alibatizwa katika mwaka wa 2002 na sasa anatumikia akiwa painia, jina ambalo Mashahidi wa Yehova huwapa waeneza-injili wao wa wakati wote. Pia, yeye ni mtumishi wa huduma katika kutaniko la Kikristo analoshirikiana nalo huko Mbang, mji mdogo kusini-mashariki mwa nchi hiyo. Tutaona ikiwa Mbilikimo wengine huko Kamerun wataamua kumwabudu Yehova, Mungu wa pekee wa kweli, anayewapenda “watu wa namna zote.”
-
-
Kuwahubiria Mbilikimo Kweli za BibliaAmkeni!—2004 | Agosti 22
-
-
[Picha katika ukurasa wa 24]
Janvier Mbaki—Mbilikimo wa kwanza kuripotiwa kuwa Shahidi—akihubiri
-