-
Ripoti ya Ulimwenguni Pote2007 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
-
-
Georgia
Mapainia wamekuwa wakihubiri katika maeneo ya mbali ya milimani nchini Georgia. Dada wawili mapainia walitembea kwa miguu kilomita nane hadi kwenye kijiji kilicho mahali ambapo barabara ya milimani inaishia, na wakaanza kuhubiri nyumba kwa nyumba. Punde mzee mmoja wa kijiji alimsimamisha Ketevan, mmoja wa dada hao, na kumuuliza kwa ukali kwa nini anahubiri hali yeye si mfuasi wa Kanisa Othodoksi. Alijaribu kumweleza lakini akakataa kusikiliza. Kisha akamwangusha chini na kumpiga kwa bakora yake. Watu wengi waliona kipigo hicho, na habari hiyo ilienea kijijini. Baadaye Ketevan alirudi kuhubiri kijijini humo. Mwanamke aliyepinga hapo awali, alimwona na kusema kwa mshangao: “Umerudi tena baada ya kipigo kile! Huo ni ujasiri ulioje! Tafadhali, njoo nyumbani kwangu unieleze zaidi.” Baada ya kusikiliza, alimwambia Ketevan kwamba amekaribishwa kumtembelea wakati wowote na kumhubiria.
-
-
Ripoti ya Ulimwenguni Pote2007 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
-
-
[Picha katika ukurasa wa 47]
Ketevan
-