-
Milenia ya Tatu Inaanza Lini?Mnara wa Mlinzi—1999 | Novemba 1
-
-
Biblia haifunui tarehe kamili ya kuzaliwa kwa Yesu. Hata hivyo, hiyo husema kwamba alizaliwa “siku za Herode mfalme.” (Mathayo 2:1) Wasomi wengi wa Biblia wanaamini kwamba Herode alikufa mwaka wa 4 K.W.K. na kwamba Yesu alizaliwa kabla ya mwaka huo—labda mapema kama mwaka wa 5 au 6 K.W.K. Wao hutegemeza mikataa yao kuhusu kifo cha Herode juu ya taarifa zilizotolewa na mwanahistoria wa karne ya kwanza Flavius Josephus.b
Kwa mujibu wa Josephus, punde tu kabla ya Mfalme Herode kufa, mwezi ulipatwa. Wasomi wa Biblia husema juu ya mwezi kupatwa kwa kiasi kidogo katika Machi 11, 4 K.W.K., kuwa uthibitisho kwamba lazima Herode alikufa mwaka huo.
-
-
Milenia ya Tatu Inaanza Lini?Mnara wa Mlinzi—1999 | Novemba 1
-
-
b Kwa mujibu wa kronolojia ya wasomi hao, milenia ya tatu ingalifika mwaka wa 1995 au wa 1996.
-