-
Milenia ya Tatu Inaanza Lini?Mnara wa Mlinzi—1999 | Novemba 1
-
-
Milenia ya Tatu Inaanza Lini?
JE, UMESIKIA dai la kwamba milenia ya tatu itaanza mwaka wa 2001 bali si mwaka wa 2000? Dai hilo ni kweli—kwa kadiri fulani. Tukisema kwamba Yesu Kristo alizaliwa katika ule uitwao sasa mwaka wa 1 K.W.K., kama wengine walivyodhania, basi Desemba 31, 2000 (wala si 1999), kwa kweli ndiyo tarehe itakayokuwa mwisho wa milenia ya pili, na Januari 1, 2001, iwe mwanzo wa milenia ya tatu.a
-
-
Milenia ya Tatu Inaanza Lini?Mnara wa Mlinzi—1999 | Novemba 1
-
-
Mwaka wa 2000 au wa 2001?
Fikiria kielezi hiki ili upate kuelewa ni kwa nini watu fulani hudai kwamba milenia ya tatu tangu Yesu azaliwe itaanza Januari 1, 2001. Tuseme unasoma kitabu chenye kurasa 200. Unapofikia mwanzo wa ukurasa wa 200, tayari umemaliza kusoma kurasa 199, kukiwa na ukurasa mmoja zaidi wa kusoma. Hutakuwa umemaliza kusoma kitabu hicho hadi ufikie mwisho wa ukurasa wa 200. Vivyo hivyo, miaka 999 ya milenia ya sasa, kama inavyohesabiwa kwa ukawaida, itakuwa imeisha Desemba 31, 1999, kukiwa kumebaki mwaka mmoja kabla ya milenia kuisha. Tukihesabu hivyo, milenia ya tatu inaanza Januari 1, 2001. Hata hivyo, jambo hilo halimaanishi kwamba siku hiyo miaka 2,000 kamili itakuwa imeisha tangu Yesu azaliwe, kama vile makala hii ionyeshavyo.
-