-
Wale Wafalme Wawili WabadilikaSikiliza Unabii wa Danieli!
-
-
16, 17. (a) Ni nani aliyekuwa mfalme wa kaskazini anayetajwa kwenye Danieli 11:25? (b) Ni nani aliyekuja kuwa mfalme wa kusini, na hilo lilitukiaje?
16 Malaika wa Mungu aliendelea na unabii huo, akisema hivi: “Naye [mfalme wa kaskazini] atachochea nguvu zake na ushujaa wake juu ya huyo mfalme wa kusini kwa jeshi kubwa; na mfalme wa kusini atafanya vita kwa jeshi kubwa mno lenye nguvu nyingi;
-
-
Wale Wafalme Wawili WabadilikaSikiliza Unabii wa Danieli!
-
-
Wakati huohuo, Malkia Septimia Zenobia wa koloni ya Roma ya Palmyra akawa mfalme wa kusini.a (Ona “Zenobia—Malkia Mpiganaji wa Palmyra,” kwenye ukurasa wa 252.) Jeshi la Palmyra lilikuwa likimiliki Misri mwaka wa 269 W.K. likisingizia kuwa lilikuwa likiifanya iwe salama kwa ajili ya Roma. Zenobia alitaka kufanya Palmyra liwe jiji kuu huko mashariki na alitaka kutawala mikoa ya mashariki ya Roma. Akishtuliwa na tamaa ya makuu ya Zenobia, Aurelian alichochea “nguvu zake na ushujaa wake” dhidi ya Zenobia.
18. Matokeo ya pambano kati ya Maliki Aurelian, mfalme wa kaskazini, na Malkia Zenobia, mfalme wa kusini yalikuwa nini?
18 Mfalme wa kusini, yaani serikali ya Zenobia, ‘alifanya’ vita dhidi ya mfalme wa kaskazini “kwa jeshi kubwa mno lenye nguvu nyingi” chini ya majenerali wawili, Zabdas na Zabbai. Lakini Aurelian aliteka Misri kisha akafunga safari kwenda Asia Ndogo na Siria. Zenobia alishindwa huko Emesa (kuitwako Homs leo), akakimbia na kwenda Palmyra. Aurelian alipolizingira jiji hilo, Zenobia alilipigania kufa na kupona lakini hakufanikiwa. Yeye na mwanaye wakakimbia kuelekea Uajemi, wakakamatwa na Waroma kwenye Mto Eufrati. Watu wa Palmyra walisalimisha jiji lao mwaka wa 272 W.K. Aurelian hakumuua Zenobia, hilo likimfanya avutie watu wengi katika ule msafara wa ushindi kupitia Roma mwaka 274 W.K. Aliishi maisha yake yaliyosalia akiwa mke Mroma.
-