-
Ustadi wa Kuogelea wa SamoniAmkeni!—2010 | Desemba
-
-
Fikiria hili: Samoni hawakati katikati ya maji hayo yenye msukosuko. Badala yake, wanapoogelea dhidi ya mkondo wa maji, wao huhifadhi nishati yao kwa kutumia mawimbi ya maji yanayozunguka kwa kasi mkondo wa maji unapokatizwa na miamba, matawi, au vitu vingine. Mawimbi hayo yanapotokea pande zote mbili za kizuizi, samoni hupinda-pinda mwili wake na kupitia katikati ya mawimbi hayo. (Ona picha.) Vikundi fulani vya samaki huogelea kwenye mawimbi yanayofanyizwa na samaki wanaoogelea mbele yao. Zaidi ya hilo, samaki wanaweza kuogelea kwenye mawimbi wanayotokeza wao wenyewe!
Watafiti wanatumaini kutumia ustadi wa kuogelea wa samoni ili kutokeza nishati kutoka kwa maji yanayoenda polepole. Kwa kawaida, mashini ya kutokeza umeme majini hutokeza umeme katika maji yanayosonga kwa mwendo wa kilomita 9.3 kwa saa, au kwa kasi zaidi. Sasa mashini inayofanyiza mawimbi ya maji inaweza kutokeza umeme katika maji yanayotiririka polepole kwa mwendo wa kilomita 3.7 kwa saa.a Hata hivyo, teknolojia hiyo haiwezi kufikia ustadi wa kuogelea wa samaki kama samoni. Profesa Michael Bernitsas wa Chuo Kikuu cha Michigan, Marekani anakiri hivi: “Hadi sasa, hatujafikia ustadi wa samoni.”
-
-
Ustadi wa Kuogelea wa SamoniAmkeni!—2010 | Desemba
-
-
a Hayo ni matumaini mazuri kwa kuwa maji mengi duniani husafiri kwa mwendo wa kilomita 5.5 kwa saa.
-