Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Msiba Wakumba Visiwa Vya Solomon
    Mnara wa Mlinzi—2008 | Mei 1
    • Tsunami Inakuja

      Patson Baea alikuwa kwenye kisiwa chao cha Sepo Hite, kilomita sita hivi kutoka Gizo, wakati tetemeko la nchi lilipotokea. Ni nini kilichowapata Patson na familia yake wakati wa msiba huo?

      Patson anasema hivi kuhusu tukio hilo: “Nilikimbia kwenye ufuo kuelekea mahali ambapo mke wangu, Naomi, na watoto wetu wanne walipokuwa. Waliangushwa chini na tetemeko hilo lakini walikuwa salama. Watoto walikuwa wakitetemeka, na wengine wao walikuwa wakilia. Mara moja mimi na Naomi tuliwatuliza.

      “Niligundua kwamba bahari ilikuwa ikisukasuka kwa njia isiyo ya kawaida. Ilikuwa wazi kwamba tsunami inakuja. Kisiwa chetu kidogo kilikabili hatari ya kufagiliwa na maji. Mama yangu, Evalyn, ambaye aliishi kwenye kisiwa kidogo cha karibu, alikuwa pia hatarini. Mara moja niliamuru familia yangu iingie ndani ya mtumbwi wetu ili twende kumwokoa.

      “Baada ya kusafiri kwa muda mfupi, wimbi kubwa sana la maji lilipita chini ya mtumbwi wetu. Bahari iliyumbayumba na kusukasuka. Tulipofika, mama alikuwa ameshtuka na kuchanganyikiwa sana hivi kwamba aliogopa kuingia ndani ya maji. Naomi na Jeremy, mwana wetu mwenye umri wa miaka 15, waliingia ndani ya maji hayo yenye nguvu na kumsaidia kuogelea ili afike kwenye mtumbwi. Kisha, tuliendesha mtumbwi huo kwa kasi sana kurudi baharini.

      “Kufikia sasa maji ya bahari yalikuwa yamepungua sana hivi kwamba miamba ya bahari ilikuwa inaonekana katika visiwa vyote. Kwa ghafula, wimbi kubwa sana la maji lilikuja na kufurika kwenye visiwa vyote viwili. Nyumba yetu ya wageni iliyo kando ya bahari iling’olewa kutoka kwenye misingi yake na kuvunjwa-vunjwa kabisa. Maji yaliingia katika nyumba yetu na kuharibu vitu vyetu vingi. Maji ya bahari yalipopungua, tuliokoa Biblia na vitabu vya nyimbo kutoka katika nyumba yetu iliyoharibika, kisha tukarudi Gizo.”

      Vitu viliharibiwa kwenye ufuo na watu wengi walikufa. Upande wa magharibi wa Kisiwa cha Ghizo ndio ulioharibiwa zaidi. Vijiji 13 hivi vya upande huo vilifagiliwa na wimbi la maji lenye urefu wa mita tano!

      Usiku huo, watu 22 walikusanyika katika Jumba la Ufalme la Mashahidi wa Yehova huko Gizo ili kuadhimisha Ukumbusho wa kifo cha Yesu. Inafurahisha kwamba hakuna yeyote kati yao aliyeumia sana kutokana na msiba huo. Ron aliyetajwa mwanzoni anasema hivi: “Hakukuwa na umeme, na taa zetu za mafuta zilikuwa zimevunjika. Kwa hiyo, Ndugu Shaw alitoa hotuba akitumia tochi. Tukiwa gizani, tuliimba nyimbo za kumshukuru Yehova kwa sauti kubwa mbalimbali zenye kuvutia.”

  • Msiba Wakumba Visiwa Vya Solomon
    Mnara wa Mlinzi—2008 | Mei 1
    • [Picha katika ukurasa wa 15]

      Uharibifu uliosababishwa na tsunami huko Gizo

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki