-
Michael Servetus—Alitafuta Ukweli Akiwa Peke YakeAmkeni!—2006 | Mei
-
-
Kutafuta Ukweli wa Kisayansi
Kwa kuwa alilazimika kuwakimbia watesaji wake, Servetus alibadili jina lake kuwa Villanovanus naye akaishi Paris, ambako alipata digrii ya sanaa na tiba. Udadisi wake wa mambo ya kisayansi ulimwongoza apasue miili ya wanadamu ili ajifunze jinsi inavyotenda kazi. Hivyo, yaelekea Servetus alikuwa Mzungu wa kwanza kufafanua mfumo wa mzunguko wa damu katika mapafu. Ufafanuzi wake umezungumziwa katika kitabu chake The Restitution of Christianity. Servetus alitoa maelezo hayo miaka 75 kabla ya William Harvey kufafanua mfumo kamili wa mzunguko wa damu.
-
-
Michael Servetus—Alitafuta Ukweli Akiwa Peke YakeAmkeni!—2006 | Mei
-
-
[Picha katika ukurasa wa 20]
Servetus alichunguza mfumo wa mzunguko wa damu katika mapafu
[Hisani]
Anatomie descriptive et physiologique, Paris, 1866-7, L. Guérin, Editor
-