Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Tafsiri ya King James—Jinsi Ilivyokuja Kuwa Maarufu
    Amkeni!—2011 | Desemba
    • Baadaye, Biblia iliyotokezwa inayoitwa English Revised Version ilipofanyiwa masahihisho machache nchini Marekani, ilichapishwa ikiwa na jina American Standard Version.b

  • Tafsiri ya King James—Jinsi Ilivyokuja Kuwa Maarufu
    Amkeni!—2011 | Desemba
    • [Sanduku/Picha katika ukurasa wa 23]

      BIBLIA YA AMERICAN STANDARD VERSION

      Biblia ya American Standard Version ilichapishwa katika mwaka wa 1901. Biblia hiyo ilitegemea maandishi ya King James Version. Inasema hivi katika dibaji yake: “Tunaelewa kwamba watu walipendezwa na Authorized [King James] Version kwa sababu ya maneno yake yenye kupendeza. Na hatupuuzi jambo hilo.” Hata hivyo, American Standard Version ilifanya rekebisho fulani muhimu.

      Dibaji yake inaeleza hivi: “Baada ya kufanya uchunguzi kwa uangalifu, wasahihishaji wa American Standard Version, walifikia kauli moja kwamba ushirikina wa Wayahudi wa kwamba jina la Mungu ni takatifu sana lisiweze kutamkwa, haupaswi kuathiri tafsiri za Agano la Kale katika Kiingereza au lugha nyingine, kama vile haukuathiri tafsiri kadhaa za wamishonari wa kisasa.”

      Si kwamba jina la Mungu, Yehova, halipatikani kabisa katika tafsiri ya King James. Linapatikana katika mistari minne, yaani, Kutoka 6:3; Zaburi 83:18; Isaya 12:2; na Isaya 26:4. Ingawa hivyo, American Standard Version ya 1901 ilirudisha jina hilo katika sehemu 7,000 hivi ambapo linastahili kuwepo.

      [Picha]

      1901

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki