-
Michezo Mipya ya KompyutaAmkeni!—2002 | Desemba 22
-
-
Michezo ya Internet Imepamba Moto
Nchi ya Britannia ina wakazi 230,000. Wakazi hao ni watu wa aina zote—wanajeshi, washonaji wa nguo, wafua-vyuma, na wanamuziki. Wao hupigana vita, hujenga majiji, hufanya biashara, huoa na kuolewa, na kufa. Lakini nchi hiyo ya Britannia ni ya kuwaziwa tu. Wachezaji huona nchi hiyo ya zama za kati katika mchezo fulani wa Internet wanaposhindana na wachezaji wengine kwa wakati uleule. Mchezo huo umependwa na wengi na unatarajiwa “kupamba moto” hata zaidi katika biashara ya michezo ya kompyuta. Mchezo unaoitwa Ultima Online—ambao unatia ndani nchi hiyo ya kuwaziwa ya Britannia—ulianzishwa mwaka wa 1997 na ndio mchezo wa kwanza wa Internet. Tangu wakati huo, michezo mingineyo ya Internet imetokea, na mingine ingali inatayarishwa.
Michezo ya Internet inatofautianaje na michezo mingine ya kompyuta? Wahusika mbalimbali katika michezo hiyo hawaendeshwi kwa kompyuta, bali wanaendeshwa na wachezaji wengine ambao wanacheza wakati huohuo kupitia Internet. Maelfu ya watu wanaweza kucheza pamoja wakati uleule. Kwa mfano, inasemekana kwamba wakati fulani mchezo wa Ultima Online ulichezwa na watu kutoka nchi 114 wakati uleule. Huenda michezo hiyo inapendwa kwa sababu watu hupata nafasi ya kushirikiana. Wachezaji wanaweza kuwasiliana, na hilo linawafanya wahisi kwamba wao ni watu wa jamii moja.
-
-
Michezo Mipya ya KompyutaAmkeni!—2002 | Desemba 22
-
-
Kulingana na shirika la Forrester Research, kila siku zaidi ya watu milioni moja huanza kucheza michezo mbalimbali ya Internet na yasemekana kwamba faida inayotokana na michezo hiyo itaongezeka wakati mbinu mpya ya kuwaunganisha watu haraka kwenye Internet itakapotumiwa katika sehemu nyingi.
-