Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Kuchapa na Kugawanya Neno Takatifu la Mungu Mwenyewe
    Mashahidi wa Yehova—Wapiga-Mbiu wa Ufalme wa Mungu
    • Mwaka uo huo, Watch Tower Society ilimiliki mabamba ya kuchapia ya The Emphatic Diaglott, yanayotia ndani maandiko ya Kigiriki ya J. J. Griesbach ya Maandiko ya Kigiriki ya Kikristo (chapa ya 1796-1806) pamoja na tafsiri ya Kiingereza ya mistari kati ya mistari. Pamoja na hiyo kulikuwa na fasili ya maandiko ya Benjamin Wilson mzaliwa wa Uingereza, aliyekuwa akiishi Geneva, Illinois, Marekani. Mabamba hayo na haki ya kuwa wachapaji pekee yalikuwa yamenunuliwa na kisha Sosaiti ikapewa kuwa zawadi. Baada ya nakala ambazo tayari zilikuwa katika akiba kuweza kupelekewa watu, mipango ilifanywa na Sosaiti ili nakala zaidi zitokezwe, na hizo zilipatikana katika 1903.

  • Kuchapa na Kugawanya Neno Takatifu la Mungu Mwenyewe
    Mashahidi wa Yehova—Wapiga-Mbiu wa Ufalme wa Mungu
    • Kuchapa Biblia Kwenye Matbaa Yetu Wenyewe

      Ilikuwa miaka 36 baada ya Watch Tower Bible and Tract Society kuanza kutangaza Biblia kwa mara ya kwanza, kwamba iliweza kuchapa na kujalidi Biblia katika kiwanda chayo yenyewe. Biblia ya kwanza kutokezwa hivyo ilikuwa The Emphatic Diaglott, ambayo mabamba yayo yalikuwa mali ya Sosaiti kwa miaka 24. Katika Desemba 1926 Biblia hiyo ilichapwa kwenye matbaa-tambarare katika kiwanda cha Sosaiti cha Concord Street katika Brooklyn. Kufikia sasa, 427,924 yazo zimetokezwa.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki