-
Mungu Afanya Agano na AbrahamuBiblia—Ina Ujumbe Gani?
-
-
Katika agano alilofanya pamoja na Abrahamu, Yehova alimwahidi kwamba atamfanya kuwa taifa kubwa, na kwamba familia zote za dunia zitajibariki kupitia kwake, nao uzao wake utaimiliki nchi ya Kanaani.
-
-
Mungu Afanya Agano na AbrahamuBiblia—Ina Ujumbe Gani?
-
-
Yehova Mungu alimhakikishia Abrahamu baadaye kwamba uzao wake ungeongezeka na kuwa kama nyota za mbinguni. Abrahamu aliamini ahadi hiyo. Hata hivyo, Sara, mke wake mpendwa hakuwa na mtoto. Kisha, Abrahamu alipokuwa na umri wa miaka 99, naye Sara akikaribia umri wa miaka 90, Mungu alimwambia Abrahamu kwamba Sara atapata mtoto. Maneno ya Mungu yalitimia. Sara akamzaa Isaka. Abrahamu alikuwa na watoto wengine, hata hivyo, yule Mkombozi aliyeahidiwa katika Edeni angetokana na ukoo wa Isaka.
-