Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Uvumbuzi Wenye Kushangaza Katika Ikweta ya Dunia
    Amkeni!—2005 | Desemba 22
    • Ili kuadhimisha mwaka wa 200 tangu wanasayansi hao Wafaransa walipofunga safari ya kwenda Ekuado, mnara wa ukumbusho ulijengwa karibu na Quito, mji mkuu wa Ekuado mnamo 1936. Mnara huo umesimamishwa kwenye mstari ambao wanasayansi hao Wafaransa wa karne ya 18 walifikiri kuwa ndio ikweta. Hadi leo, watalii hutembelea mnara huo unaoitwa, Katikati ya Dunia. Wakiwa hapo wanaweza kukanyaga pande mbili za dunia zinazotenganishwa na ikweta. Lakini je, hilo ni kweli?

      La! Uvumbuzi wa hivi karibuni unaonyesha kwamba mstari wa ikweta uko mbali kidogo na mahali hapo. Kwa kushangaza, karne nyingi kabla ya wanasayansi Wafaransa waliotumwa kuchunguza nadharia ya Newton kufika huko, wenyeji wa eneo hilo walikuwa tayari wamegundua mahali hususa ambapo mstari huo ulipaswa kuwa. Hilo lingewezekanaje?

      Ikweta Halisi

      Mnamo 1997, magofu ya ukuta wa nusu duara yaliyoonekana kuwa hayana maana yoyote yalivumbuliwa kwenye kilele cha Mlima Catequilla, ambao uko kaskazini kidogo ya Quito. Kwa kutumia mfumo wa kupokea habari kutoka kwa setilaiti (GPS), mchunguzi, Cristóbal Cobo aligundua kwamba mwisho mmoja wa ukuta huo ulikuwa umejengwa kabisa kwenye ikweta.b

  • Uvumbuzi Wenye Kushangaza Katika Ikweta ya Dunia
    Amkeni!—2005 | Desemba 22
    • b Kwa upande mwingine, kulingana na mfumo wa GPS, mnara maarufu wa ukumbusho wa Katikati ya Dunia uko meta 300 hivi kusini ya ikweta halisi.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki