-
Kuponda Kichwa cha NyokaUfunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
Mahakimu kwa Miaka Elfu Moja
8, 9. Sasa Yohana hutuambia nini juu ya wale wanaoketi juu ya viti vya ufalme, nao ni akina nani?
8 Baada ya miaka elfu, Shetani anaachiliwa kutoka katika abiso kwa kitambo kifupi. Kwa nini? Kabla ya kutoa jibu, Yohana anarudisha uangalifu wetu kwenye mwanzo wa kipindi hicho cha wakati. Tunasoma: “Na mimi niliona viti vya ufalme, na kulikuwako wale walioketi juu yavyo, na nguvu za kuhukumu zilipewa kwao.” (Ufunuo 20:4a, NW) Ni nani hawa wanaoketi juu ya viti vya ufalme na kutawala katika mbingu pamoja na Yesu aliyetukuzwa?
9 Wao ni “watakatifu” ambao Danieli alieleza habari yao kuwa wakitawala katika Ufalme pamoja na Mmoja aliye “kama mwana wa binadamu.” (Danieli 7:13, 14, 18, NW) Wao ndio wale wale wazee 24 wanaoketi juu ya viti vya ufalme vya kimbingu katika kuwapo hasa kwa Yehova. (Ufunuo 4:4) Wao ni kutia ndani mitume 12, ambao Yesu aliwapa ahadi hii: “Katika uumbaji-upya wakati Mwana wa binadamu anaketi chini juu ya kiti cha ufalme chake chenye utukufu, nyinyi ambao mmefuata mimi mtaketi nyinyi wenyewe pia juu ya viti vya ufalme kumi na viwili, mkihukumu makabila kumi na mawili ya Israeli.” (Mathayo 19:28, NW) Wangetia ndani Paulo pia, pamoja na Wakristo Wakorintho ambao walibaki wakiwa waaminifu. (1 Wakorintho 4:8; 6:2, 3) Wao ni kutia ndani, vilevile, washiriki wa kundi la Laodikia ambao walishinda.—Ufunuo 3:21.
10. (a) Sasa Yohana huelezaje habari ya wafalme 144,000? (b) Kutokana na aliyotuambia Yohana mapema zaidi, wafalme 144,000 hutia ndani nani?
10 Viti vya ufalme—144,000 vyote pamoja—vimetayarishwa kwa ajili ya hawa washindi wapakwa-mafuta ambao ‘wamenunuliwa kutoka miongoni mwa aina ya binadamu wakiwa matunda ya kwanza kwa Mungu na kwa Mwana-Kondoo.’ (Ufunuo 14:1, 4, NW)
-
-
Kuponda Kichwa cha NyokaUfunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
13. (a) Inatupasa tuoneje miaka elfu ambayo katika hiyo 144,000 hutawala, na kwa nini? (b) Papiasi wa Hierapolisi aliionaje miaka elfu? (Ona kielezi cha chini.)
13 Kutawala na kuhukumu kwao kutakuwa kwa miaka elfu moja. Je! hii ni miaka elfu moja halisi, au inatupasa tuione kwa njia ya ufananisho kuwa ni kipindi kirefu cha wakati, kisichodhihirishwa? “Maelfu” yaweza kumaanisha hesabu kubwa isiyodhihirishwa, kama vile kwenye 1 Samweli 21:11. Lakini hapa “elfu” ni halisi, kwa kuwa inaonekana mara tatu katika Ufunuo 20:5-7 kama ile “miaka elfu.” Paulo aliita wakati huu wa hukumu “siku moja” alipotaarifu: “Yeye [Mungu] ameweka siku moja ambayo katika hiyo yeye anakusudia kuhukumu dunia inayokaliwa kwa uadilifu.” (Matendo 17:31, NW) Kwa kuwa Petro anatuambia kwamba siku moja kwa Yehova ni kama miaka elfu moja, inafaa kwamba hii Siku ya Hukumu iwe miaka elfu moja halisi.c—2 Petro 3:8, NW.
-
-
Kuponda Kichwa cha NyokaUfunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
Wakiwa mahakimu kwa miaka elfu moja, wao, pamoja na Yesu, wataongoza kwa upendo wanadamu waitikifu kuelekea mradi wa uhai wa milele.—Yohana 3:16.
-