-
Ndoa Ambayo Inanufaisha Mamilioni Wanaoishi SasaMnara wa Mlinzi—1989 | Julai 1
-
-
12. Jambo hilo lilikamilishwaje nyumbani kwa Rebeka?
12 Rebeka alipiga mbio kwa msisimuko mwingi akaenda nyumbani kuambia jamaa yao. Baadaye, baba na ndugu ya Rebeka waliposikia kutoka kinywani mwa Eliezeri mwenyewe kusudi la safari yake na jinsi Yehova alivyokuwa amejibu sala yake, walikubali bila kusita-sita kwamba Rebeka anapaswa kuwa mke wa Isaka. “Ikawa kwamba wakati mtumishi wa Abrahamu alipokuwa amesikia maneno yao, mara hiyo alijisujudisha ardhini mbele za Yehova. Na mtumishi huyo akaanza kutoa vitu vya fedha na vitu vya dhahabu na mavazi na kumpa Rebeka; na yeye akawapa ndugu yake na mama yake vitu viteule.”—Mwanzo 24:52, 53, NW.
-
-
Ndoa Ambayo Inanufaisha Mamilioni Wanaoishi SasaMnara wa Mlinzi—1989 | Julai 1
-
-
16. (a) Kwa kufaa, mtumishi wa Abrahamu alikuwaje picha ya roho takatifu ya Mungu? (b) Ni swali gani linaloweza kuulizwa kuhusu roho na bibi-arusi?
16 Jina la Eliezeri linamaanisha “Mungu Wangu Ni Msaidiaji.” Kwa jina na matendo, kwa kufaa yeye ni picha ya roho takatifu ya Abrahamu Mkubwa Zaidi, Yehova Mungu, ambayo Yeye alipeleka kwenye bara hili la mbali, dunia yetu, ili kuchagua bibi-arusi anayefaa kwa ajili ya Isaka Mkubwa Zaidi, Yesu Kristo. (Yohana 14:26; 15:26, NW) Jamii ya bibi-arusi ni “lile kundi,” linalojumlika kuwa hivyo kutokana na wanafunzi wa Yesu ambao wamezaliwa kwa roho takatifu wakiwa wana wa kiroho wa Mungu. (Waefeso 5:25-27; Warumi 8:15-17) Sawa na vile Rebeka alivyopokea zawadi za bei kubwa, ndivyo washiriki wa kwanza wa kundi la Kikristo siku ya Pentekoste 33 W.K. walivyopokea zawadi za kimuujiza kuthibitisha wito wao wa kimungu. (Matendo 2:1-4) Kama Rebeka, wao wameyaacha kwa nia mahusiano yote ya kilimwengu na ya kimnofu ili hatimaye waungane pamoja na Bwana-arusi wao wa kimbingu. Kuanzia wakati ambapo washiriki mmoja mmoja wa jamii ya bibi-arusi wanaitwa mpaka kifo chao, ni lazima wao walinde ubikira wao wa kiroho wanapokuwa wakisafiri kupita katika ulimwengu wa Shetani ulio hatari na wenye utongozi. (Yohana 15:18, 19; 2 Wakorintho 11:3; Yakobo 4:4) Ikiwa imejawa na roho takatifu, jamii ya bibi-arusi inawaalika wengine kwa uaminifu washiriki maandalizi ya Yehova kwa ajili ya wokovu. (Ufunuo 22:17) Je! wewe unafuata kielelezo cha bibi-arusi huyo kwa kuuitikia pia mwelekezo wa roho hiyo?
-