Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Ndoa Ambayo Inanufaisha Mamilioni Wanaoishi Sasa
    Mnara wa Mlinzi—1989 | Julai 1
    • 13. Uchaguzi wa Yehova ulitiliwaje nguvu kuwa ulifaa?

      13 Rebeka alilionaje pendeleo la kuchaguliwa kimungu awe bibi-arusi wa Isaka? Kesho yake jambo fulani lilitukia ili lifunue hisia za kweli alizokuwa nazo kwa ndani. Akiisha kutimiza kusudi la safari yake, Eliezeri alitamani kurudia bwana wake bila ukawivu. Lakini jamaa za Rebeka wakataka bibi-arusi akae pamoja nao angalau siku kumi. Kwa hiyo Rebeka akaachiwa aamue kama alikuwa tayari kuondoka mara hiyo. “Mimi nina nia ya kwenda,” akasema. Kwa kukubali kuacha jamaa zake mara hiyo na kufunga safari kwenda nchi ya mbali ili akafunge ndoa na mwanamume asiyepata kumwona kamwe, yeye alionyesha imani nyingi ajabu katika mwelekezo wa Yehova. Hiyo ilitilia nguvu uhakika wa kwamba alikuwa ndiye mchaguliwa anayefaa.​—Mwanzo 24:54-58, NW.

  • Ndoa Ambayo Inanufaisha Mamilioni Wanaoishi Sasa
    Mnara wa Mlinzi—1989 | Julai 1
    • 15. (a) Tunaona kielelezo gani kizuri sana katika Eliezeri, Rebeka, na wenye kumtumikia? (b) Usimulizi huu unatangulia kuwa kivuli cha nini?

      15 Eliezeri, Rebeka, na mabibi wenye kumtumikia waliutegemea kikamili mwelekezo wa Yehova, hicho kikiwa ni kielelezo kizuri sana kwa Wakristo leo! (Mithali 3:5, 6) Kwa kuongezea, usimulizi huo ni igizo lenye kuimarisha imani. Kama vile tumeona, Abrahamu alikuwa mfananishi wa Yehova Mungu, aliyetoa Mwana wake mpendwa, yule Isaka Mkubwa Zaidi, ili wanadamu wenye dhambi waweze kupata uhai wa milele. (Yohana 3:16) Utayarishaji wa ndoa ya Isaka ulifanywa muda fulani baada ya yeye kuponyoshwa kwenye kifo juu ya madhabahu. Ulikuwa unabii wa utayarishaji wa ndoa ya kimbingu, ambao ulianza kwa bidii baada ya ufufuo wa Yesu.

      Ndoa ya Isaka Mkubwa Zaidi

      16. (a) Kwa kufaa, mtumishi wa Abrahamu alikuwaje picha ya roho takatifu ya Mungu? (b) Ni swali gani linaloweza kuulizwa kuhusu roho na bibi-arusi?

      16 Jina la Eliezeri linamaanisha “Mungu Wangu Ni Msaidiaji.” Kwa jina na matendo, kwa kufaa yeye ni picha ya roho takatifu ya Abrahamu Mkubwa Zaidi, Yehova Mungu, ambayo Yeye alipeleka kwenye bara hili la mbali, dunia yetu, ili kuchagua bibi-arusi anayefaa kwa ajili ya Isaka Mkubwa Zaidi, Yesu Kristo. (Yohana 14:26; 15:26, NW) Jamii ya bibi-arusi ni “lile kundi,” linalojumlika kuwa hivyo kutokana na wanafunzi wa Yesu ambao wamezaliwa kwa roho takatifu wakiwa wana wa kiroho wa Mungu. (Waefeso 5:25-27; Warumi 8:15-17) Sawa na vile Rebeka alivyopokea zawadi za bei kubwa, ndivyo washiriki wa kwanza wa kundi la Kikristo siku ya Pentekoste 33 W.K. walivyopokea zawadi za kimuujiza kuthibitisha wito wao wa kimungu. (Matendo 2:1-4) Kama Rebeka, wao wameyaacha kwa nia mahusiano yote ya kilimwengu na ya kimnofu ili hatimaye waungane pamoja na Bwana-arusi wao wa kimbingu. Kuanzia wakati ambapo washiriki mmoja mmoja wa jamii ya bibi-arusi wanaitwa mpaka kifo chao, ni lazima wao walinde ubikira wao wa kiroho wanapokuwa wakisafiri kupita katika ulimwengu wa Shetani ulio hatari na wenye utongozi. (Yohana 15:18, 19; 2 Wakorintho 11:3; Yakobo 4:4) Ikiwa imejawa na roho takatifu, jamii ya bibi-arusi inawaalika wengine kwa uaminifu washiriki maandalizi ya Yehova kwa ajili ya wokovu. (Ufunuo 22:17) Je! wewe unafuata kielelezo cha bibi-arusi huyo kwa kuuitikia pia mwelekezo wa roho hiyo?

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki