Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • “Tafadhali Sikilizeni Ndoto Hii”
    Mnara wa Mlinzi—2014 | Agosti 1
    • Bila kujua nia yao, Yosefu aliwakaribia, akitarajia kukutana nao kwa amani. Badala yake, ndugu zake walimshambulia! Ghafula wakamvua vazi lake la pekee, wakampeleka kwenye kisima kilichokauka, na kumsukuma ndani. Yosefu akaanguka shimoni puu! Akatulia kidogo, kisha akajikaza kusimama, lakini hangeweza kamwe kutoka ndani. Aliona tu anga kupitia tundu la kisima na kusikia sauti za ndugu zake. Aliwalilia na kuwasihi, lakini wakampuuza. Bila kujali, walikula chakula hapo karibu. Rubeni alipoondoka, walizungumzia tena kuhusu kumuua mvulana huyo, lakini Yuda akawashauri wamuuze kwa wafanyabiashara waliokuwa wakipita karibu. Eneo la Dothani lilikuwa karibu na barabara ya kwenda Misri, na punde si punde msafara wa Waishmaeli na Wamidiani ukaja. Kabla Rubeni hajarudi, tayari walikuwa wamemuuza. Walimuuza ndugu yao awe mtumwa kwa shekeli 20.b—Mwanzo 37:23-28; 42:21.

      Ndugu za Yosefu wakimtupa ndani ya shimo na kuchukua vazi lake

      Yosefu alifanya yaliyo sawa, lakini ndugu zake walimchukia

  • “Tafadhali Sikilizeni Ndoto Hii”
    Mnara wa Mlinzi—2014 | Agosti 1
    • b Hata kuhusu jambo hili dogo, Biblia ni sahihi kabisa. Hati za nyakati hizo zinaonyesha kwamba bei ya mtumwa ilikuwa shekeli 20 huko Misri.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki