Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Kuhifadi Uhai Katika Wakati wa Njaa
    Mnara wa Mlinzi—1987 | Mei 1
    • 16. (a) Ni wapi tu “chakula” cha kuhifadhi uhai kinapopatikana leo? (b) Kupanda “nafaka” kwa ajili ya wanadamu waliotaabishwa sana kwa njaa kumepanuliwaje?

      16 Kwenye mkono wa kuume wa Yehova yuko Msimamizi wa Chakula wake, akiwa Mfalme aliyetawazwa, Yesu mtukuzwa. (Matendo 2:34-36) Kama vile ilivyowalazimu watu kujiuza wenyewe wawe watumwa ili waendelee kuwa hai, ndivyo ilivyo lazima leo wote wanaotaka kuendelea kuishi wamjie Yesu, wawe wafuasi wake waliojiweka wakfu kwa Mungu. (Luka 9:23, 24) Kama vile Yakobo alivyowaelekeza wana wake wamwendee Yusufu wakapate chakula, ndivyo Yehova anavyowatolea mwongozo wanadamu wenye kutubu wamwendee Mwana wake mpendwa, Yesu Kristo. (Yohana 6:44, 48-51) Yesu ana-wakusanya wafuasi wake ndani ya makundi yaliyo kama miji​—zaidi ya 52,000 katika se-hemu zote za ulimwengu leo​—ambamo wana-lishwa kutokana na wingi wa chakula cha kiroho na kutolewa mfuriko wa “nafaka”, kama “mbegu” ya kupanda shambani. (Mwanzo 47:23, 24; Mathayo 13:4-9, 18-23) Mashahidi hao wa Yehova ni wafanya kazi wenye nia kweli kweli! Wengi zaidi na zaidi kati yao wanajitolea kwa utumishi wa painia wa wakati wote, na wengi kufikia 595,896 kati yao walishiriki, wakiwa kilele, katika kazi hiyo iliyopendelewa katika mwezi mmoja mwaka jana. Huo unakuwa wastani wa mapainia zaidi ya 11 katika kila kundi!

  • Kuhifadi Uhai Katika Wakati wa Njaa
    Mnara wa Mlinzi—1987 | Mei 1
    • 21. (a) Ni pendeleo gani kubwa tunalofurahia leo? (b) Inatupasa tushukuru kwa jambo gani, nasi tunaweza kuonyesha asante zetu jinsi gani?

      21 Leo, chini ya mwelekezo wa Yusufu Mkubwa Zaidi, Yesu Kristo, sisi tuna pendeleo kubwa la kukusanywa tuingie ndani ya makundi yaliyo kama miji. Humo tunaweza kula karamu ya wingi wa chakula cha kiroho na pia kupanda mbegu za ukweli na kuzieneza habari njema za kwamba chakula cha kiroho kinapatikana. Tunafanya hivyo kwa manufaa ya wote wanaoyakubali masharti na maandalizi yaliyopangwa kwa upendo na Mtawala Mwenye Enzi Kuu, Yehova. Tunaweza kuwa wenye shukrani kama nini kwa Mungu wetu kwa ajili ya zawadi ya Mwana wake, Yusufu Mkubwa Zaidi, anayetumikia akiwa Msimamizi wa chakula cha kiroho mwenye hekima! Yeye ndiye amekabidhiwa na Yehova kutenda akiwa Mhifadhi uhai katika wakati huu wa njaa ya kiroho. Kila mmoja wetu na aonyeshe bidii katika kutoa utumishi mtakatifu kwa kufuata mfano wake na akiwa chini ya uongozi wake!

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki