Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Ufalme wa Mungu Watawala
    Ujuzi Uongozao Kwenye Uhai Udumuo Milele
    • 9 Vivyo hivyo, Yehova hutupa sisi uhakikishio wa uhalisi wa Ufalme. Kama vile ionyeshwavyo kwenye Kitabu cha Biblia cha Waebrania, sehemu nyingi za Sheria zilitangulia kuonyesha mpango wa Ufalme. (Waebrania 10:1) Mimweko ya kimbele ya Ufalme wa Mungu ilikuwa wazi pia katika ufalme wa kidunia wa Israeli. Hiyo haikuwa serikali ya kawaida, kwani watawala waliketi juu ya “kiti cha enzi cha BWANA [“Yehova,” NW].” (1 Mambo ya Nyakati 29:23) Zaidi ya hayo, ilikuwa imetabiriwa hivi: “Fimbo ya enzi haitaondoka katika Yuda, wala mfanya sheria kati ya miguu yake hata atakapokuja Yeye [“Shilo,” NW], mwenye milki, ambaye mataifa watamtii.” (Mwanzo 49:10)a Ndiyo, Yesu, aliye Mfalme wa kudumu wa serikali ya Mungu, angezaliwa katika nasaba hiyo ya wafalme wa Kiyudea.—Luka 1:32, 33.

  • Ufalme wa Mungu Watawala
    Ujuzi Uongozao Kwenye Uhai Udumuo Milele
    • a Jina Shilo lamaanisha “Yeye Ambaye Ni Yake; Yeye Ambaye Ni Mali Yake.” Baada ya muda fulani, ikawa wazi kwamba “Shilo” alikuwa ni Yesu Kristo, “Simba aliye wa kabila ya Yuda.” (Ufunuo 5:5) Baadhi ya Targum za Kiyahudi ziliweka tu “Mesiya” au “Mesiya mfalme” mahali pa neno “Shilo.”

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki