Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Je, Inafaa Wakristo Kuhifadhi maiti kwa Kuipaka Dawa?
    Mnara wa Mlinzi—2002 | Machi 15
    • Je, Inafaa Wakristo Kuhifadhi maiti kwa Kuipaka Dawa?

      Mzee mwaminifu wa ukoo Yakobo alipokaribia kufa, alitoa ombi hili la mwisho: “Mnizike pamoja na baba zangu, katika pango iliyomo shambani mwa Efroni, Mhiti katika ile pango iliyomo shambani mwa Makpela, iliyo mbele ya Mamre katika nchi ya Kanaani.”—Mwanzo 49:29-31.

      YOSEFU aliheshimu ombi la baba yake kwa kufuata desturi iliyoenea huko Misri wakati huo. Aliwaagiza “watumishi wake, waganga kwamba wampake babaye dawa asioze.” Kulingana na Mwanzo sura ya 50, waganga walichukua siku 40 kuitayarisha maiti kama ilivyokuwa desturi. Kupakwa dawa kwa maiti ya Yakobo kuliwezesha msafara mkubwa wa familia yake pamoja na watu mashuhuri kutoka Misri kusafiri mwendo wa kilometa 400 kupeleka maiti hiyo kuizika huko Hebroni.—Mwanzo 50:1-14.

      Je, inawezekana kwamba siku moja mwili wa Yakobo uliopakwa dawa utapatikana? Uwezekano wa kupatikana kwa mwili huo ukiwa katika hali nzuri ni mdogo sana. Jambo linalofanya vitu vingi vya kale visipatikane katika Israeli ni kwamba eneo hilo lina maji mengi. (Kutoka 3:8) Vifaa vya chuma na mawe vinapatikana kwa wingi, lakini vingine vilivyo hafifu kama nguo, ngozi, na miili iliyopakwa dawa vimeharibiwa na unyevunyevu na mabadiliko ya muda mrefu.

  • Je, Inafaa Wakristo Kuhifadhi maiti kwa Kuipaka Dawa?
    Mnara wa Mlinzi—2002 | Machi 15
    • Mwili wa Yakobo ulipakwa dawa na watu ambao imani yao ilikuwa tofauti na yake. Hata hivyo hatuwezi kuwazia Yosefu akiwapa waganga mwili wa babaye, na kutaka watoe sala na kufuata desturi zilizoambatana na kupaka maiti dawa huko Misri wakati huo. Yakobo na Yosefu walikuwa wanaume wenye imani. (Waebrania 11:21, 22) Maandiko hayashutumu kuhifadhiwa kwa mwili wa Yakobo kwa kupakwa dawa ingawa Yehova hakuagiza jambo hilo lifanywe. Kupakwa dawa kwa mwili wa Yakobo ili kuuhifadhi hakukukusudiwa kuwe kielelezo kwa taifa la Israeli au kwa kutaniko la Kikristo. Kwa hivyo, hakuna maagizo hususa kuhusu jambo hilo katika Neno la Mungu. Baada ya mwili wa Yosefu kuhifadhiwa kwa kupakwa dawa huko Misri, desturi hiyo haitajwi tena katika Maandiko.—Mwanzo 50:26.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki