-
Mungu Akusudia Kwamba Mwanadamu Aone Shangwe ya Maisha Katika ParadisoMnara wa Mlinzi—1989 | Agosti 1
-
-
10, 11. (a) Ni wazi kwamba Adamu alijifunza mambo gani ya uhakika, lakini ni maswali gani mengine aliyohitaji kujibiwa? (b) Baba wa kimbingu alimpa Adamu majibu gani?
10 Akili ya Adamu yenye ufahamivu mwingi, yenye ubichi wa kutaka kujua mambo ilifyonza habari hizi kwa hamu nyingi. Sasa yeye alijua kwamba hakutoka kwenye makao hayo yasiyoonekana ambako Mfanyi na Mfanyizi wake alikuwa akinenea. Bali, yeye alifanyizwa kutokana na ardhi aliyokuwa akiishi na kwa hiyo alikuwa wa kiardhi. Mpaji-Uhai na Baba yake alikuwa Yehova Mungu. Yeye alikuwa “nafsi hai.” Alikuwa “mwana wa Mungu” kwa maana alikuwa amepokea uhai wake kutoka kwa Yehova Mungu. Miti iliyokuwa kandokando yake katika bustani ya Edeni ilizaa matunda yaliyokuwa mazuri kwa chakula, ili ayale na kuendelea kuwa hai akiwa nafsi yenye uhai. Na hata hivyo, kwa nini iwe lazima aendelee kuwa hai, na kwa nini aliwekwa duniani, katika bustani hii ya Edeni? Yeye alikuwa mwanadamu aliyefanyika kikamili akiwa na akili ya kuelewa mambo na mwenye uwezo mbalimbali wa kimwili, naye alistahili kujua. Ama sivyo, yeye angewezaje kutimiza kusudi lake maishani na hivyo afurahishe Mfanyi na Baba yake kwa kutenda penzi la kimungu? Majibu ya maswali haya yanayofaa yalitolewa katika habari inayofuata:
-
-
Mungu Akusudia Kwamba Mwanadamu Aone Shangwe ya Maisha Katika ParadisoMnara wa Mlinzi—1989 | Agosti 1
-
-
b Mnabii Musa, aliyeandika habari hiyo katika kitabu cha Mwanzo katika karne ya 16 kabla ya Wakati wa Kawaida wetu, aliongezea habari inayofuata kuhusu mto huu wa Kiedeni, kulingana na maarifa yaliyokuwako katika siku yake:
“Jina la wa kwanza ni Pishoni; ndio unaozunguka nchi yote ya Havila, ambako kuna dhahabu; na dhahabu ya nchi ile ni njema; huko kuna bedola, na vito shoham. Na jina la mto wa pili ni Gihoni; ndio unaozunguka nchi yote ya Kushi. Na jina la mto wa tatu ni Hidekeli; ndio unaopita mbele ya Ashuru. Na mto wa nne ni Frati.”—Mwanzo 2:11-14.
-