Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Kwa Nini Mungu Anaruhusu Watu Wateseke?
    Mnara wa Mlinzi—2014 | Januari 1
    • Sophia: Sawa. “Basi nyoka alikuwa mwenye kujihadhari kuliko wanyama wote wa mwituni ambao Yehova Mungu alikuwa amewafanya. Kwa hiyo akaanza kumwambia mwanamke: ‘Je, ni kweli kwamba Mungu alisema msile matunda ya kila mti wa bustani?’ Mwanamke akamjibu na kumwambia nyoka: ‘Tunaweza kula matunda ya miti ya bustani. Lakini kuhusu kula matunda ya mti ulio katikati ya bustani, Mungu amesema, “Msiyale, wala msiyaguse ili msife.”’ Ndipo nyoka akamwambia mwanamke: ‘Hakika hamtakufa. Kwa maana Mungu anajua kwamba siku ileile mtakapokula matunda yake macho yenu yatafunguliwa, nanyi mtakuwa kama Mungu, mkijua mema na mabaya.’”

  • Kwa Nini Mungu Anaruhusu Watu Wateseke?
    Mnara wa Mlinzi—2014 | Januari 1
    • Michelle: Kweli kabisa. Ona sasa madai yasiyo ya kweli ambayo Shetani alitoa kumhusu Mungu. Alisema: “Hakika hamtakufa.” Shetani alikuwa akidai kwamba Mungu ni mwongo!

      Sophia: Sijawahi kusikia jambo hilo.

      Michelle: Shetani alipodai kwamba Mungu ni mwongo, alitokeza suala ambalo lingehitaji wakati ili kutatuliwa. Unajua ni kwa nini?

      Sophia: Aaah, sijui.

      Michelle: Labda nitumie mfano kuelezea jambo hilo. Tuseme siku moja ninakuja kwako na kudai kwamba nina nguvu kuliko wewe. Ungethibitishaje hilo si kweli?

      Sophia: Ningekupa mtihani.

      Michelle: Kweli kabisa. Labda tungetafuta chombo kizito na kuona ni nani kati yetu anayeweza kukiinua.Kwa kweli ni rahisi kuthibitisha ni nani aliye na nguvu kuliko mwingine.

      Sophia: Ninaelewa unachomaanisha.

      Michelle: Lakini namna gani ikiwa badala ya kusema nina nguvu, nidai kwamba mimi ni mnyoofu na wewe si mnyoofu? Hilo ni jambo ngumu kuthibitisha, sivyo?

      Sophia: Ndiyo.

      Michelle: Kwa kweli, tofauti na nguvu, unyoofu si jambo linaloweza kuthibitishwa kwa urahisi.

      Sophia: Ni kweli.

      Michelle: Bila shaka, njia rahisi ya kusuluhisha hilo ingekuwa kuacha wakati upite ili wengine wajionee ni nani kati yetu aliye mnyoofu.

      Sophia: Umesema kweli.

      Michelle: Sasa, angalia tena simulizi hili katika kitabu cha Mwanzo. Je, Shetani alidai kwamba ana nguvu kuliko Mungu?

      Sophia: La.

      Michelle: Mungu angethibitisha jambo hilo haraka. Lakini Shetani alidai kwamba ni mnyoofu na Mungu si mnyoofu. Ni kana kwamba alimwambia Hawa, ‘Mungu anawadanganya, lakini mimi ninakuambia ukweli.’

      Sophia: Hilo linashangaza.

      Michelle: Kwa hekima, Mungu alijua kwamba njia bora ya kusuluhisha dai hilo ni kuacha wakati upite. Mwishowe, ingejulikana ni nani aliyesema ukweli na ni nani aliyesema uwongo.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki