-
Kwa Nini Mungu Anaruhusu Watu Wateseke?Mnara wa Mlinzi—2014 | Januari 1
-
-
Sophia: Sawa. “Basi nyoka alikuwa mwenye kujihadhari kuliko wanyama wote wa mwituni ambao Yehova Mungu alikuwa amewafanya. Kwa hiyo akaanza kumwambia mwanamke: ‘Je, ni kweli kwamba Mungu alisema msile matunda ya kila mti wa bustani?’ Mwanamke akamjibu na kumwambia nyoka: ‘Tunaweza kula matunda ya miti ya bustani. Lakini kuhusu kula matunda ya mti ulio katikati ya bustani, Mungu amesema, “Msiyale, wala msiyaguse ili msife.”’ Ndipo nyoka akamwambia mwanamke: ‘Hakika hamtakufa. Kwa maana Mungu anajua kwamba siku ileile mtakapokula matunda yake macho yenu yatafunguliwa, nanyi mtakuwa kama Mungu, mkijua mema na mabaya.’”
-
-
Kwa Nini Mungu Anaruhusu Watu Wateseke?Mnara wa Mlinzi—2014 | Januari 1
-
-
Michelle: Kwa njia fulani, lilithibitisha. Hata hivyo madai ya Shetani yalihusisha mengi. Tazama tena mstari wa 5. Unaona Shetani alimwambia Hawa jambo gani lingine?
Sophia: Alimwambia kwamba ikiwa angekula matunda hayo, macho yake yangefunguliwa.
Michelle: Ndiyo, na kwamba angekuwa ‘kama Mungu, akijua mema na mabaya.’ Kwa hiyo Shetani alidai kwamba Mungu alikuwa akiwanyima wanadamu mambo mazuri.
Sophia: Ninaelewa sasa.
Michelle: Na hilo pia lilikuwa dai zito sana.
Sophia: Unamaanisha nini?
Michelle: Shetani alidai kwamba Hawa—na wanadamu wote kwa ujumla—wangekuwa na maisha mazuri bila kuongozwa na Mungu. Katika kisa hiki pia, Yehova alijua kwamba njia nzuri ya kushughulikia mambo ni kumwacha Shetani athibitishe madai yake. Hivyo, Mungu amemruhusu Shetani autawale ulimwengu huu kwa muda fulani. Hilo linaonyesha ni kwa nini wanadamu wanateseka sana—Shetani ndiye hasa mtawala wa ulimwengu huu, bali si Mungu.d Lakini kuna habari njema.
-