Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Mtegemee Yehova Ili Kupata Faraja
    Mnara wa Mlinzi—1996 | Novemba 1
    • 5 Kwa njia hiyo, hao wenzi wenye dhambi wakaanza kufa. Alipokuwa akitangaza hukumu ya kifo, Mungu alitaarifu hivi pia kwa Adamu: “Ardhi imelaaniwa kwa ajili yako; kwa uchungu utakula mazao yake siku zote za maisha yako; michongoma na miiba itakuzalia, nawe utakula mboga za kondeni.” (Mwanzo 3:17, 18) Hivyo Adamu na Hawa wakapoteza lile taraja la kuifanya dunia ambayo haikuwa imelimwa iwe paradiso. Wakiwa wamefukuzwa kutoka Edeni, walilazimika kutumia nishati zao ili kujitahidi kupata chakula kutoka kwenye ardhi iliyolaaniwa. Wazao wao, wakiwa wamerithi hali hiyo yenye dhambi na kufa, wakaja kuwa na uhitaji mkubwa wa kupata faraja.—Warumi 5:12.

  • Mtegemee Yehova Ili Kupata Faraja
    Mnara wa Mlinzi—1996 | Novemba 1
    • 8 Yehova alikusudia kuuharibu ulimwengu huo mwovu kupitia furiko la kitufe, lakini kwanza akamwagiza Noa ajenge safina ili kuhifadhi uhai. Hivyo, jamii ya kibinadamu na aina za wanyama zikaokolewa. Noa na familia yake lazima wawe walihisi wametulizwa kama nini baada ya hilo Furiko walipokuwa wakitoka nje ya safina na kuingia dunia iliyosafishwa! Ilifariji kama nini kukuta kwamba ile laana juu ya ardhi ilikuwa imeondolewa, ikifanya utendaji wa kilimo uwe rahisi zaidi sana! Kwa kweli, unabii wa Lameki ulithibitika kuwa kweli, na Noa aliishi kulingana na maana ya jina lake. (Mwanzo 8:21) Akiwa mwabudu mwaminifu wa Mungu, Noa alitumika katika kuletea wanadamu kiasi fulani cha “faraja.” Hata hivyo, ule uvutano mwovu wa Shetani na roho wake waovu haukuishia na Furiko, nao wanadamu huendelea kuugua chini ya mzigo wenye kulemea wa dhambi, ugonjwa, na kifo.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki