Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Kumtolea Yehova Dhabihu Zenye Kukubalika
    Mnara wa Mlinzi—1999 | Februari 1
    • Yehova alisababu na Kaini. “Kwa nini una ghadhabu? na kwa nini uso wako umekunjamana?” akauliza. Swali hilo lilimpa Kaini fursa ya kutosha kuchunguza hisia zake na nia yake. “Kama ukitenda vyema,” Yehova akaendelea kusema, “hutapata kibali? Usipotenda vyema dhambi iko, inakuotea mlangoni, nayo inakutamani wewe, walakini yapasa uishinde.”—Mwanzo 4:6, 7. (Ona sanduku kwenye ukurasa wa 23.)

  • Kumtolea Yehova Dhabihu Zenye Kukubalika
    Mnara wa Mlinzi—1999 | Februari 1
    • Kabla na baada ya Abeli kuuawa kimakusudi, Kaini alikataa ‘kutenda vyema.’ Aliamua kuacha dhambi imshinde, na kwa sababu hiyo, Kaini akafukuzwa kutoka eneo ambalo familia ya kibinadamu iliishi. “Alama,” labda agizo rasmi tu, iliwekwa ili mtu yeyote asilipize kisasi kifo cha Abeli kwa kumwua Kaini.—Mwanzo 4:15.

  • Kumtolea Yehova Dhabihu Zenye Kukubalika
    Mnara wa Mlinzi—1999 | Februari 1
    • “KWA nini una ghadhabu? na kwa nini uso wako umekunjamana?” Kwa swali hilo, Yehova alisababu na Kaini kwa fadhili. Hakumlazimisha Kaini abadilike, kwa kuwa Kaini alikuwa na uhuru wa kuchagua. (Linganisha Kumbukumbu la Torati 30:19.) Hata hivyo, Yehova hakusita kumwonyesha Kaini matokeo ya mwenendo wake mpotovu. Alimwonya Kaini hivi: “Kama ukitenda vyema, hutapata kibali? usipotenda vyema dhambi iko, inakuotea mlangoni, nayo inakutamani wewe.”—Mwanzo 4:6, 7.

      Yafaa kuangaliwa kwamba hata alipomtolea karipio hilo kali, Yehova hakumtendea Kaini kama ‘mtu asiyeweza kunufaika na msaada.’ Badala yake, alimwambia Kaini baraka ambazo angepata kama angezibadili njia zake, naye alionyesha uhakika wa kwamba Kaini angeweza kushinda tatizo hilo kama angeamua kufanya hivyo. “Ukitenda vyema,” Yehova akasema, “hutapata kibali?” Pia alimwuliza Kaini hivi kuhusu ghadhabu yake ya kutaka kuua kimakusudi: ‘Je, utaishinda?’

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki