Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Tembea Pamoja na Mungu Nyakati Hizi za Misukosuko
    Mnara wa Mlinzi—2005 | Septemba 1
    • 10, 11. (a) Uovu ulieneaje baada ya Adamu na Hawa kuasi? (b) Enoko alihubiri ujumbe gani wa kinabii, na watu waliitikiaje?

      10 Kwa mfano, fikiria jinsi ambavyo uovu ulienea haraka katika jamii ya wanadamu baada ya Adamu kutenda dhambi. Biblia inatueleza kwamba mwana mzaliwa wa kwanza wa Adamu, Kaini, ndiye aliyekuwa mwanadamu wa kwanza kuua alipomuua ndugu yake Abeli. (Mwanzo 4:8-10) Baada ya Abeli kuuawa kikatili, Adamu na Hawa walipata mwana mwingine, nao wakamwita Sethi. Tunasoma hivi kumhusu: “Sethi akazaa mwana pia naye akamwita jina lake Enoshi. Wakati huo watu wakaanza kuliitia jina la Yehova.” (Mwanzo 4:25, 26) Inasikitisha kwamba huko “kuliitia jina la Yehova” kulifanywa kwa njia ya kumwasi Yehova.b Miaka mingi baada ya Enoshi kuzaliwa, mzao fulani wa Kaini aliyeitwa Lameki alitunga wimbo kwa ajili ya wake zake wawili na kutangaza kwamba alikuwa amemuua kijana aliyemtia jeraha. Kisha Lameki akaonya hivi: “Ikiwa Kaini atalipizwa kisasi mara 7, basi Lameki ni mara 77.”—Mwanzo 4:10, 19, 23, 24.

  • Tembea Pamoja na Mungu Nyakati Hizi za Misukosuko
    Mnara wa Mlinzi—2005 | Septemba 1
    • b Kabla ya siku za Enoshi, Yehova alizungumza na Adamu. Abeli alimtolea Yehova toleo lililokubalika. Pia, kabla Kaini hajachochewa kuua kwa sababu ya hasira yenye wivu, Mungu alizungumza naye. Hivyo, yaonekana watu walianza “kuliitia jina la Yehova” kwa njia mpya, si katika ibada safi.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki