Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Mtegemee Yehova Ili Kupata Faraja
    Mnara wa Mlinzi—1996 | Novemba 1
    • 6. (a) Ni ahadi gani yenye kufariji ambayo Mungu alitoa baada ya wanadamu kutumbukia katika dhambi? (b) Lameki alitoa unabii gani juu ya faraja?

      6 Alipokuwa akimhukumu mwanzilishi wa uasi wa mwanadamu, Yehova alithibitika kuwa ‘Mungu apaye faraja.’ (Warumi 15:5) Alifanya hivyo kwa kuahidi kutuma “mbegu” ambayo hatimaye ingekomboa wazao wa Adamu kutokana na matokeo yenye msiba ya uasi wa Adamu. (Mwanzo 3:15) Baada ya muda, Mungu aliandaa pia mimweko ya kimbele ya ukombozi huo. Kwa kielelezo, alimpulizia Lameki, mzao wa mbali wa Adamu kupitia mwana wake Sethi, atabiri juu ya jambo ambalo mwana wa Lameki angefanya: “Huyu ndiye atakayetufariji kwa kazi yetu na kwa taabu ya mikono yetu katika nchi aliyoilaani BWANA.” (Mwanzo 5:29) Kwa kupatana na ahadi hiyo, mvulana huyo aliitwa Noa, jina lielewekalo kumaanisha “Pumziko” au “Kitulizo.”

  • Mtegemee Yehova Ili Kupata Faraja
    Mnara wa Mlinzi—1996 | Novemba 1
    • 8 Yehova alikusudia kuuharibu ulimwengu huo mwovu kupitia furiko la kitufe, lakini kwanza akamwagiza Noa ajenge safina ili kuhifadhi uhai. Hivyo, jamii ya kibinadamu na aina za wanyama zikaokolewa. Noa na familia yake lazima wawe walihisi wametulizwa kama nini baada ya hilo Furiko walipokuwa wakitoka nje ya safina na kuingia dunia iliyosafishwa! Ilifariji kama nini kukuta kwamba ile laana juu ya ardhi ilikuwa imeondolewa, ikifanya utendaji wa kilimo uwe rahisi zaidi sana! Kwa kweli, unabii wa Lameki ulithibitika kuwa kweli, na Noa aliishi kulingana na maana ya jina lake. (Mwanzo 8:21) Akiwa mwabudu mwaminifu wa Mungu, Noa alitumika katika kuletea wanadamu kiasi fulani cha “faraja.” Hata hivyo, ule uvutano mwovu wa Shetani na roho wake waovu haukuishia na Furiko, nao wanadamu huendelea kuugua chini ya mzigo wenye kulemea wa dhambi, ugonjwa, na kifo.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki