-
Simulizi la Noa na Gharika Kuu—Je, Ni Hekaya Tu?Maswali ya Biblia Yajibiwa
-
-
Safina ya Noa ilionekanaje?
Safina ilikuwa sanduku kubwa lenye umbo la mstatili lenye urefu wa mita 133, upana wa mita 22, na kimo cha mita 13.a Ilijengwa kutokana na mbao za mti wenye utomvu, na ikafunikwa kwa lami ndani na nje. Ilikuwa na ghorofa tatu na ilikuwa na vyumba kadhaa. Kulikuwa na mlango ubavuni mwake na inaelekea kulikuwa na dirisha upande wa juu. Inaelekea pia ilikuwa na paa lililoinuka katikati kwa kadiri fulani ili kuruhusu maji yatiririke.—Mwanzo 6:14-16.
-
-
Simulizi la Noa na Gharika Kuu—Je, Ni Hekaya Tu?Maswali ya Biblia Yajibiwa
-
-
a Biblia inataja vipimo vya safina kwa kutumia mikono. “Kipimo cha kawaida cha mkono katika Kiebrania kilikuwa sentimita 44.45.”—The Illustrated Bible Dictionary, Toleo Lililorekebishwa, Sehemu ya 3, ukurasa wa 1635.
-