Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • “Mambo Yaliyofunuliwa Ni Yetu Sisi”
    Mnara wa Mlinzi—1986 | Mei 15
    • 4, 5. Ni mafunuo gani zaidi ambayo Yehova alitoa, na ni akina nani waliokuwa mifereji aliyoitumia?

      4 Bila shaka wanaume na wanawake wenye kumwogopa Mungu walikuwa na maulizo mengi juu ya Uzao huo. Yeye angekuwa nani? Angefika wakati gani? Angefaidije wanadamu? Karne zilipoendelea kupita, Yehova alitoa mafunuo zaidi juu ya makusudi yake, na hatimaye akajibu maulizo yote hayo. Kabla ya Gharika, alimwongoza Enoki kwa roho Yake atabiri katika unabii juu ya uharibifu uliokuwa unakuja wa uzao wa Shetani. (Yuda 14, 15) Karibu miaka 2,400 kabla ya Wakati wa Kawaida wetu, alimkabidhi Noa ufunuo wa kwamba uhai na damu ya kibinadamu ni vitu vitakatifu—ukweli ambao ungekuwa wa maana kubwa wakati Uzao ulioahidiwa ungefika.—Mwanzo 9:1-7.

  • “Mambo Yaliyofunuliwa Ni Yetu Sisi”
    Mnara wa Mlinzi—1986 | Mei 15
    • 11, 12. Ni nini yaliyokuwa baadhi ya mafunuo mazuri ajabu yaliyotolewa kupitia mfereji huo mpya?

      11 Uhakika mkubwa wa hizo ‘siri takatifu’ mpya ulikuwa kwamba Yesu Kristo, ule Uzao ulioahidiwa, alikuwa ametokea. (Wagalatia 3:16) Yesu alikuwa ndiye “Shilo,” yule mwenye haki ya kutawala wanadamu, na Yehova alimweka rasmi awe Mfalme wa Ufalme ambao hatimaye ungerudisha Paradiso kwenye dunia hii. (Isaya 11:1-9; Luka 1:31-33) Yesu alikuwa pia ndiye Kuhani Mkuu aliyewekwa rasmi na Yehova, ambaye alitoa uhai wake mkamilifu usio na kidoa uwe ukombozi kwa ajili ya wanadamu, hayo yakiwa ni matumizi mazuri ajabu ya ile kanuni ya utakatifu wa damu. (Waebrania 7:26; 9:26) Tangu wakati huo, wanadamu wenye kuamini walikuwa na tumaini la kupata tena uhai mkamilifu wa kibinadamu uliopotezwa na Adamu.—1 Yohana 2:1, 2.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki