-
Mwe na Imani Kama ya Abrahamu!Mnara wa Mlinzi—2001 | Agosti 15
-
-
6, 7. Abramu na Sarai walijikuta katika hali gani zenye kuhuzunisha, naye Yehova alimwokoaje Sarai?
6 Jambo hilo liliwahuzunisha kama nini Abramu na Sarai! Ilionekana kwamba Sarai alikuwa karibu kunajisiwa. Isitoshe, kwa kutojua kwamba Sarai alikuwa ameolewa, Farao alimpa Abramu zawadi nyingi sana, hivi kwamba “alikuwa na kondoo na ng’ombe , na punda waume, na watumwa, na wajakazi, na punda wake, na ngamia.”b (Mwanzo 12:16) Ni lazima Abramu awe alichukizwa kama nini na zawadi hizo! Ingawa hali zilionekana kuwa mbaya, Yehova hakuwa amemwacha Abramu.
-
-
Mwe na Imani Kama ya Abrahamu!Mnara wa Mlinzi—2001 | Agosti 15
-
-
b Huenda ikawa Hagari, ambaye baadaye alikuwa suria wa Abramu, alikuwa mmojawapo wa watumishi ambao Abramu alipewa wakati huo.—Mwanzo 16:1.
-