Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Kudumisha Umoja wa Kikristo Katika Mahusiano ya Kibiashara
    Mnara wa Mlinzi—1986 | Novemba 15
    • Umaana wa Mapatano Rasmi

      5. Jambo lililopata Abrahamu katika kununua shamba linaonyeshaje ubora wa kuwa na mapatano rasmi?

      5 Ili kusaidia kuzuia hali za kutoelewana katika shughuli za kibiashara, fikiria jinsi Abrahamu alivyonunua kipande cha shamba. Yeye “akampimia Efroni ile fedha aliyotaja masikioni mwa bani Hethi, shekeli za fedha mia nne ya namna inayotumika na wenye biashara. Basi shamba la Efroni lililokuwa katika Makpela . . . viliyakinishwa kuwa mali yake [Abrahamu], mbele ya bani Hethi, mbele ya watu wote waingiao katika mlango wa mji wake.” Hayo hayakuwa mapatano ya faraghani yenye kufanywa kwa uungwana wa wanaume ati. Yalikuwa mapatano rasmi, yaliyoyakinishwa (yaliyothibitishwa) mbele ya mashahidi. Hakukuwa na kutokuelewana juu ya kilichokuwa kimenunuliwa na bei barabara iliyotolewa.​—Mwanzo 23:2-4, 14-18.

      6. Wakristo wanaweza kufanyaje shughuli za kibiashara za maana ziwe rasmi?

      6 Vivyo hivyo, ni jambo la hekima Wakristo wafanye shughuli za maana ziwe rasmi. Ikiwa shughuli yenyewe inahusu kuuza bidhaa fulani, wanaohusika wanaweza kuandika kilichouzwa, bei yacho,njia itakayotumiwa kulipa wakati na jinsi gani bidhaa hiyo itakavyopelekwa, na masharti mengine yaliyokubaliwa. Ikiwa linalohusika ni utumishi fulani unaopasa kufanywa, wanaohusika wanaweza kuandika ni kazi gani itakayofanywa, ni wakati gani inapopasa kumalizwa, bei kwa kuifanya, na mambo mengine. Hati hiyo inayoandikwa inapasa iwe na tarehe na kutiwa sahihi, na nakala inapasa iwekwe na pande zote mbili zinazohusika. Mapatano hayo yaliyoandikwa ni ya maana sana hasa katika biashara ya kishirika. Inasaidia watu wa pande zote mbili waelewe uhusiano wao waziwazi na kuwasaidia waishi kupatana na shauri hili la Yesu: “Maneno yenu yawe Ndiyo, ndiyo; Siyo, siyo.”’(Mathayo 5:37) Katika mambo yanayohusu hali zilizo ngumu zaidi kushughulikiwa, inaweza kufaa zaidi kutafuta msaada wa wastadi wa kibiashara katika kutayarisha mapatano yanayoandikwa.

  • Kudumisha Umoja wa Kikristo Katika Mahusiano ya Kibiashara
    Mnara wa Mlinzi—1986 | Novemba 15
    • [Picha katika ukurasa wa 16]

      Abrahamu alithibitisha ununuzi wa nchi kwa mapatano rasmi pamoja na Efroni

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki