-
Nguvu ya SalaMnara wa Mlinzi—2000 | Machi 1
-
-
ELIEZERI anaamini kwamba sala ni yenye nguvu. Kwa imani yenye kutokeza, iliyo kama ya mtoto, yeye aomba hivi kwa unyenyekevu: “Ee BWANA, Mungu wa bwana wangu Ibrahimu, nakuomba mambo yangu uyajalie yawe heri leo, ukamfadhili bwana wangu Ibrahimu. Tazama! nimesimama karibu na kisima cha maji, na binti za watu wa mjini wanatoka kuteka maji, basi na iwe hivi; yule msichana nitakayemwambia, Tua mtungi wako, nakuomba, ninywe; naye akasema, Unywe, nami natawanywesha na ngamia zako pia; basi huyu na awe ndiye uliyemchagulia mtumishi wako Isaka; na kwa hayo nitajua ya kuwa umemfadhili bwana wangu.”—Mwanzo 24:12-14.
-
-
Nguvu ya SalaMnara wa Mlinzi—2000 | Machi 1
-
-
Tunaweza kujifunza mengi kutokana na sala ya Eliezeri. Sala hiyo ilionyesha imani yake yenye kutokeza, unyenyekevu, na kuhangaikia mahitaji ya wengine bila ubinafsi. Sala ya Eliezeri pia ilionyesha ujitiisho wake kwa njia ambayo Yehova hushughulika na wanadamu. Yaelekea alijua uhusiano wa pekee uliokuwapo kati ya Abrahamu na Mungu na vilevile ahadi Yake kwamba wanadamu wote wangebarikiwa wakati ujao kupitia Abrahamu. (Mwanzo 12:3) Hivyo, Eliezeri alianza sala yake kwa maneno haya: “Ee BWANA, Mungu wa bwana wangu Ibrahimu.”
-