-
Kitu Chenye Thamani Zaidi Kuliko Hazina za MisriMnara wa Mlinzi—2002 | Juni 15
-
-
Malezi na Elimu
Yokebedi “akamtwaa mtoto, akamnyonyesha. Mtoto akakua naye akamleta kwa binti Farao, akawa mwanawe.” (Kutoka 2:9, 10) Biblia haisemi Musa aliishi na wazazi wake muda mrefu kadiri gani. Watu fulani hufikiri kwamba wazazi wa Musa walikaa naye hadi alipoachishwa kunyonya—miaka miwili au mitatu—lakini huenda ikawa walikaa naye muda mrefu zaidi ya huo. Kitabu cha Kutoka kinasema tu ‘alikua’ pamoja na wazazi wake, jambo ambalo halidokezi umri hususa. Vyovyote vile, Amramu na Yokebedi walitumia wakati huo kumweleza mwana wao kwamba yeye ni Mwebrania na kumfundisha kuhusu Yehova. Mafanikio yao katika kusitawisha imani na kupenda uadilifu katika moyo wa Musa yangeonekana baadaye.
-
-
Kitu Chenye Thamani Zaidi Kuliko Hazina za MisriMnara wa Mlinzi—2002 | Juni 15
-
-
[Sanduku katika ukurasa wa 11]
Mapatano na Akina Mama Walioajiriwa Kunyonyesha
Kwa kawaida akina mama waliwanyonyesha watoto wao. Hata hivyo, msomi Brevard Childs asema hivi katika Journal of Biblical Literature, “nyakati fulani familia za kifalme [nchi za Mashariki ya Kati] ziliajiri mama wa kunyonyesha. Desturi hiyo ilikuwa ya kawaida wakati ambapo mama hakuweza kumnyonyesha mtoto wake au wakati ambapo mama hakujulikana. Mama wa kunyonyesha alichukua jukumu hilo la kumlea mtoto na vilevile kumnyonyesha kwa kipindi hususa.” Hati kadhaa za mafunjo zinazoonyesha mapatano yaliyofanywa na akina mama wa kunyonyesha zimepatikana katika mabaki ya vitu vya kale huko Mashariki ya Kati. Hati hizo zinathibitisha desturi hiyo iliyokuwa imeenea sana kuanzia utawala wa Wasumeria hadi mwisho-mwisho wa utawala wa Wagiriki huko Misri. Mambo yanayotajwa katika hati hizo yanatia ndani taarifa za wahusika, kipindi cha kunyonyesha, hali za kazi, chakula walichopaswa kula, faini ambayo mtu angelipa kwa kuvunja mapatano, mishahara, na jinsi ambavyo mishahara ingelipwa. Kwa kawaida, “utunzaji uliendelea kwa muda unaozidi miaka miwili hadi mitatu,” asema Childs. “Mama wa kunyonyesha alimlea mtoto nyumbani mwake, lakini nyakati nyingine alipaswa kumrudisha mtoto kwa mwenyewe ili achunguzwe.”
-